@bongofive: Dodoma: Mbunge wa Katavi, Thomas Kampala, amesema vita dhidi ya ushoga ni jambo linalopaswa kupewa kipaumbele na kila mmoja, akieleza kuwa vitendo hivyo vinakwenda kinyume na maadili ya jamii. Kampala amesema yupo katika mchakato wa kukutana na wanasheria kwa ajili ya kujadili mapendekezo ya marekebisho ya sheria, akitaka hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya vitendo anavyovitaja kuwa ni vya ushoga. Amesema miongoni mwa mapendekezo hayo ni kuwepo kwa adhabu kwa mtu atakayebainika kujihusisha na vitendo vya ushoga, akisisitiza kuwa suala hilo linahitaji kushughulikiwa kwa nguvu zaidi. Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumzia umuhimu wa kulinda maadili ya jamii na kukabiliana na vitendo anavyodai vinaendelea kuenea. Imeandaliwa na @yasiningitu