@bashasha_tv: DODOMA:Mama mmoja na mtoto wake mwenye umri wa miaka mitatu wamefariki dunia baada ya kujeruhiwa katika ajali ya moto iliyotokea jana jioni, Septemba 3, 2026, katika Kata ya Kizota, Jijini Dodoma. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Diwani wa Kata ya Kizota, Jamal Ngalya, amesema chanzo cha moto huo kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika eneo la fundi wa uchomeleaji (welding). Kwa mujibu wa Ngalya, mama huyo pamoja na mtoto wake walijeruhiwa katika tukio hilo na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu, lakini baadaye walifariki dunia wakiwa hospitalini. Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma, Mrakibu (SF) Rehema Menda, amewashukuru na kuwapongeza wananchi wa Kizota kwa kuwa watulivu na kushirikiana na Jeshi hilo wakati wa zoezi la uokoaji na uzimaji wa moto. Menda amesema ushirikiano wa wananchi ulikuwa muhimu katika kuwezesha shughuli za uokoaji na udhibiti wa moto kufanyika kwa ufanisi. #bashashatvupdates #bashashadigital #bashashamedia

bashasha_tv
bashasha_tv
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 04 September 2026 06:38:22 GMT
15385
517
20
41

Music

Download

Comments

ummyfaizan2
miss Zahara 😘🥰 :
duuuh jamn kizota jamn 😭😭😭
2026-09-04 13:01:01
0
user8243865614151
rey qeen💞💞💞 :
Nachukia kuckia Au kuona mtu wa Dodoma akipata shida Mungu nilindie mkoa wangu 🥺🥺🥺🥺🥺🥺
2026-09-04 08:13:16
17
venty1214
1212 :
poleni
2026-09-04 11:24:27
0
ney.cute.baby
ney cute baby 🤩🤩 :
daah hii ajali tumeipita jana kizota maskini😭😭
2026-09-04 09:53:37
1
doricasdenis
🌹♥️dayana💕❤️ :
mmh ni wapi kipenziii
2026-09-04 07:47:27
0
dismasprivatus
dismasprivatus :
daaah pumzika kwa aman🥺🥺
2026-09-04 08:18:51
2
user2980068465981
Aisha yahaya 🥰🥰 :
nijilan yangu jaman
2026-09-04 15:53:22
0
elizabeth.fransic1
Elizabeth fransic :
𝕁𝕒𝕞𝕒𝕟𝕚 𝕞𝕟𝕘𝕦 𝕒𝕨𝕒𝕡𝕠𝕞𝕫𝕚𝕤𝕙𝕖
2026-09-04 17:28:30
0
vassycute
vassy cute... :
Daah🙏
2026-09-04 15:51:43
0
aisha.hussein075
🖇️Isha🥰🥰 :
Jamani daaa
2026-09-04 08:24:31
0
tiner042
tiner💞💜😍 :
daah!! yani roho imeniuma sana mama na uyo mtoto jana jaman kizota😢😢
2026-09-04 13:19:31
0
nemah031
Nemah :
🙆😭😭
2026-09-04 07:59:58
0
user8304460921415
grace :
mwenyezi MUNGU azilaze roho za marehemu mahali pema peponi😭😭😭😭😭😭😭 inauma sana poleni
2026-09-04 06:57:14
0
allyjuma300
@ Allyjuma123 :
daah poleni sana wafiwa na Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu
2026-09-04 07:37:53
0
dalalimrosso
DALALI_MROSSSO_DODOMA :
tumia lugha nzur ni tanesco so maneno
2026-09-04 08:51:41
0
To see more videos from user @bashasha_tv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About