@hopechanneltz: Leo tunazindua #OneVoice27! 🎉 Huu ni zaidi ya uzinduzi ni mwito wa kuingia kazini kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Katika mikono yetu tunashika kifaa chenye uwezo wa kufikia maelfu ya watu kila siku. Simu yako si kifaa cha mawasiliano tu; ni kibweta cha kidijitali kinachoweza kupeleka ujumbe wa tumaini, upendo, na wokovu kwa ulimwengu unaohitaji Yesu. Kila post, kila share, kila comment, na kila ujumbe unaotuma unaweza kuwa daraja linalomleta mtu karibu na Kristo. 📱 Tumia simu yako kwa utukufu wa Mungu. 🌍 Tumia sauti yako kufikia ulimwengu. 🤝 Ungana na maelfu ya waumini katika misheni moja. ✨ Shiriki tumaini. Shiriki Yesu. _Ongeza sauti yako kwenye Utume._ Tumaini linaanzia hapa. #OneVoice27 #TumainiLinaanziaHapa #AllThingsNew #MamboYoteMapya