@focustvtz: Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Benjamin Sitta, alijitolea kuwa mdhamini wa Mwananchi mmoja mwenye tatizo la upofu wa macho anayefahamika kwa jina la Msafiri mkaazi wa Kata ya Migoli Tarafa ya Isimani katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa, aweze kupewe Mkopo wa Serikali kiasi cha Shillingi Milioni Moja, ajiendeleze Kupitia shughuli yake ya Kilimo ili kuepuka kuwa tegemezi na kuombaomba kwenye jamii. Tukio hilo lilitokea katika Ziara ya DC Sitta iliyofanyika Septemba 04, 2026, ambapo Kupitia Ziara hiyo alipata fursa ya kushiriki Mkutano wa hadhara uliolenga kuwasikiliza na kutatua kero zinazowakabili Wananchi wa Kata ya Migori iliyopo Tarafa ya Isimani katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa. #FocusTVTanzania