@official.nunu8: 1- Kuanzia BAADA YA ALFAJIRI hadi jua linapochomoza Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas akisema: “Walinieleza watu nisio na chembe ya shaka kuhusu ukweli na uaminifu wao – na pia kwa ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuswali baada ya Alfajiri mpaka jua lichomoze, na baada ya Swalaah ya Alasiri mpaka jua lichwe. [Hadiyth Swahiyh na Al-Bukhaariy (581) na Muslim (826)]. 2- KUANZIA KUCHOMOZA KWA JUA hadi jua liwe limechomoza urefu wa mkuki juu ya upeo wa macho siku hizi hii inachukuliwa kuwa sawa na dakika kumi na mbili baada ya jua kuchomoza, lakini ili kuwa upande sahihi mtu anapaswa kuifanya ni kama robo saa. 3- WAKATI JUA LINAPOPINDUKA ADHUHURI, Ni kwa Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir (Radhwiya Allaahu Anhu) aliposema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitukataza kuswali au kuwazika maiti zetu katika nyakati tatu: Jua linapochomoza angavu mpaka lipande, jua linapokuwa katikati ya mbingu Adhuhuri mpaka lipinduke, na wakati jua linapokurubia kuchwa mpaka lichwe kabisa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (831)]. 4- Kuanzia baada ya SWALAH YA ‘ASR mpaka jua lizame. Hadiyth ya Abu Sa’iyd aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (( Hapana Swalaah baada ya Alfajiri mpaka jua lipande, na hapana Swalaah baada ya Alasiri mpaka jua lichwe)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (586) na Muslim (827)]. 5- Wakati wa KUZAMA KWA JUA kuanzia linapoanza kuzama hadi litakapozama kabisa. Nakupenda. Allaah 🙏🏾🙏🏾