@rashidbattashy: RAIS MWINYI AFUNGUA HOTEL ILIYOGHARIMU BILIONI 132 - PWANI MCHANGANI ZANZIBAR ✍🏻 @rashidbattashy Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi @dr.hmwinyi ameahidi kuwa serikali itaendelea kuboresha miundombinu ili kuhakikisha inaimarisha ukuaji wa uwekezaji nchini Rais Mwinyi ameeleza hayo wakati akifungua moja ya hotel ya nyota tano ya @kappasenseszanzibar and @anayahotelszanzibar iliyokuwepo Pwani Mchangani Mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar Amesema hatua hizo ni pamoja na kuhakikisha kunakuwepo kwa miundombinu mapya ya uboreshaji na uzalishaji wa nishati ya umeme, miundombinu ya barabara na miundombinu mengine Aidha amesema hatua hiyo pia inaongeza fursa za uzalishaji wa ajira kwa vijana ambapo mradi huo umetoa ajira zaidi ya mia tatu zikitoa kipaumbele kwa wananchi wa Zanzibar hasa wanaozunguka eneo la mradi huo Waziri wa Kazi na Uwekezaji Zanzibar Mheshimiwa @shariffashariff amesema katika kipindi cha miaka 6 cha uongozi wa Rais Mwinyi, @zipazanzibar imesajilia zaidi ya miradi 600 ikiwa ni hatua kubwa katika kufungua uchumi wa Zanzibar Mradi wa hoteli hiyo unatajwa kugharimu Dola za Marekani Milioni 50 sawa na wastani wa shilingi za Kitanzania Bilioni 132 cc: @rashidbattashy