@chawamata_tv: Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA), Shaban Matwebe, ameamua kumsaidia mama aliyesambaa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akiendesha baiskeli huku akiwa amembeba mtoto wake mgongoni. Matwebe amefikia uamuzi huo baada ya kuguswa na video ya mama huyo iliyosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, hali iliyomfanya kuamua kuchukua hatua ya kumsaidia ili kupunguza changamoto zinazomkabili katika maisha yake. Katika hatua hiyo, Matwebe amemlipia mama huyo kodi ya nyumba ya kipindi cha miaka miwili, sambamba na kumpatia kiasi cha shilingi laki tano (500,000) kwa ajili ya kumsaidia katika mahitaji yake muhimu. Aidha, kwa kushirikiana na wadau wengine, Matwebe amemuwezesha mama huyo kupata fedha za kuanzisha mtaji wa biashara, hatua inayolenga kumsaidia kujikwamua kiuchumi na kujenga maisha yenye uwezo wa kujitegemea. Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni sehemu ya juhudi za kuguswa na changamoto za wananchi wanaoonekana kupitia mitandao ya kijamii na kuchukua hatua za kuwasaidia kwa vitendo.
CHAWAMATA TV
Region: TZ
Sunday 06 September 2026 17:38:15 GMT
Music
Download
Comments
There are no more comments for this video.
To see more videos from user @chawamata_tv, please go to the Tikwm
homepage.