@uvccm_tz: *HODI MBEYA, MWENYEKITI UVCCM KAWAIDA ANAKUJA* Ni ziara ya Mwenyekiti wa UVCCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC) katika mkoa wa Mbeya kuanzia tarehe 07 Septemba 2026 akifuatilia uhai wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kuzungumza na makundi ya Vijana, kuwatembelea wanufaika wa mikopo ya Serikali na kusikiliza changamoto mbalimbali za Wananchi ili kuzifikisha sehemu husika. Mbeya ni zamu yetu, karibu Ndugu Kawaida