@sensibledigitalservices: KAPOTEZA ZAIDI YA 5M KWENYE BIASHARA YA HOTSPOT… SOMA HII KWA MAKINI ISIJE IKAKUKUTA. Kuna mzee mmoja kutoka Tanga aliamua kuingia kwenye biashara ya Hotspot akiwa na matumaini makubwa sana ya kupata pesa. Alimpa installer mmoja huduma ya kumfungia Hotspot. Installer akaja akafunga eneo lenye coverage ya karibu kilomita 2. Nilipomuuliza, “Kwa nini umeamua kufunga eneo kubwa hivi?” Akanijibu, “Niliamini nikidominate eneo kubwa nitapata pesa nyingi zaidi.” Nikamuuliza tena, “Una uhakika router unayotumia ni specific kwa ajili ya kuuza internet?” Akasema, “Hapana, ni router ya home use.” Nikamuuliza, “Una uhakika wateja wakiwa ndani ya eneo hilo wanapata huduma nzuri na stable?” Akasema, “Hapana.” Nikamuuliza swali lingine, “Unajua maana ya RECAP DATA?” Akasema, “Sijui.” Nikamuuliza swali la mwisho ambalo liliniumiza zaidi… “Wateja wako wanasemaje kuhusu huduma yako?” Akasema, “Wamesema huduma ni mbovu.” Nikamuuliza, “Ushawahi kuona router ambayo imetengenezwa specifically kwa ajili ya kuuza internet kwa watu wengi?” Akasema, “Hapana.” Nikamuangalia nikamuuliza, “Kwa hiyo umejifunza nini?” Akasema: “Nimejifunza kwamba EXPERIENCE MATTERS MORE THAN EXPECTATION.” Mzee huyu alipoteza zaidi ya 5M, si kwa sababu Hotspot ni biashara mbaya. Alipoteza kwa sababu aliingia kwenye biashara bila elimu sahihi, bila mentor mwenye experience, na akaamini kwamba kufunika eneo kubwa ndiyo maana ya kupata pesa nyingi. HELLOW MSOMAJI… Hotspot si biashara ya kununua router, kuifunga na kusubiri pesa iingie. Hotspot inahitaji maarifa, experience, location analysis, vifaa sahihi, mfumo sahihi wa billing, network management na zaidi ya yote mtu mwenye experience ya biashara hii. Usitafute tu mtu wa kuuza vifaa. Tafuta mtu anayejua biashara yenyewe. Kwa sababu installer anaweza kukufungia mfumo unaowaka, lakini mentor mwenye experience anaweza kukuambia kama huo mfumo kweli una nafasi ya kukuletea faida. Usiruhusu expectation ikufanye upuuze experience. Jifunze kwanza. Uliza maswali. Fanya research. Sikiliza watu waliokwisha kupitia njia hiyo. Maana wakati mwingine gharama ya experience inaweza kuwa ndogo sana kuliko gharama ya kufanya mistake. EXPERIENCE MATTERS MORE THAN EXPECTATION. #tanzaniantiktok🇹🇿 #fyp #creatorsearchinsights
sensible digital services
Region: TZ
Monday 07 September 2026 08:03:27 GMT
Music
Download
Comments
Juma Said Ali :
upo wapi? Unaweza ukanifanyia installation?
2026-10-12 09:15:17
0
hassanmkenga926 :
HOTSOT ndio ntuni
2026-10-11 14:36:34
0
Josephernest028 :
Hii biashara ni illigal kampuni ya simu ikiamua kukukomalia mahakamani ni hatari, hii ni kama kutumia kisimbusi cha azam tv kusambaza channels kwa wengine ni kosa kisheria.
2026-09-08 03:22:41
19
Calvinkzb :
Kuna Issues inaitwa FUP na Data Recap Sasa watu wanaingia Kwenye hii business kwa Motivation, Storytelling bila kuhitaji kujua ukweli halisi na Changamoto zake
2026-09-08 06:09:33
8
✅✅junior :
Fact kabisaa ni ishu moja tu simple aina hiyo impact wanaongeaa unawez kuta router kumbe iko limit bando afu tunalipia kama unlimite kumbe ni unlimited kwa ww
2026-09-07 17:17:24
6
🅣🅗🅔 🅞🅝🅔 :
Full stop
2026-09-17 21:58:34
2
ghost_rego :
kak mm boda boda lakin nahitaj nijifunz kabl ya kuanz plzzz kak🙏🏽
2026-09-07 23:34:29
2
ZshopExpress :
MIMI NINACHO KIONA KIKUBWA UTAFANYAA LAKIN KAMA HUNA UTUNDU MZURI WA MASWALA YA IT AU UKAPATA MTU MUAMINIFU AKAKUSIMAMAMIA BUSNESS YAKO ANAE ELEWA BASI HUTOBOI UTAKWAMA NJIANI TU 😁
2026-09-11 12:01:37
5
Moses official Company :
Fact, mkuu
2026-09-07 12:18:27
1
Jéllodz J7 :
Tatozo tamaa tengeneza, tengeneza site ya kuhudumia watu 30 tu, ndo uwezo wa router zote tz na access points, halafu rudia site kama hizo 30... Tamaa mbaya, unataka userve watu 200
2026-09-09 17:23:59
5
Code Breaker :
waambie kaka umenena vyema kaka
2026-09-21 11:43:12
2
Sato services :
brooo umeonge fact sana Sasa Fanya jamb moja ambalo kitakua safi kama utatengeneza group thn link uiweke kwenye bio ilitujiungo kwenye group tujadili vzri ama unainaje Mzee mana unachoongea ni point ☝️sana mana atamm natmani kufanya iyo kazi
2026-10-01 10:54:07
1
ONTUZU TAILOR :
namba mm nisaidie ili nifanye iyo bishala kaka
2026-09-21 12:35:54
1
HERR MNYAMA :
kaka Una kitu
2026-10-02 14:15:29
1
ᴰᵁᴰᵁᵁ_ᴹᴱᴺᴰᴱᶻ :
kabisa kaka
2026-09-10 00:15:54
1
Caldezar Saucedo El Puno :
Sahihi
2026-09-16 18:14:47
1
Ezekieli Alnordy :
kabsa kaka
2026-09-21 11:07:35
1
Kafira masumbuko :
nitumie namba yako kaka
2026-09-07 20:53:59
1
diamaskamala :
bro be my mentor
2026-09-07 17:36:27
1
Emmy brand :
sahihi
2026-10-16 06:47:52
0
MELANÉ LUXE 🤎 :
Kweli kbs
2026-10-06 12:14:09
0
azizaalmas8 :
nahitaji nifungue hii biashara mwezi ujao kaka naomba maelekezo
2026-10-14 18:33:50
0
mzungu ni Mungu :
ila umeongea kwel
2026-10-07 09:51:25
0
HOCK TZ :
hata mimi akili yangu inaniambia fanya hii biashara lakini usifanye bila kupata mwalimu na uelewa wa kutosha
2026-10-01 17:28:14
0
Bando kitonga :
aa
2026-10-01 10:48:56
0
To see more videos from user @sensibledigitalservices, please go to the Tikwm
homepage.