@chawamata_tv: VIDEO: WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ameanguka ghafla wakati akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa kutafakari hali ya kisiasa nchini Tanzania. Warioba alikuwa miongoni mwa wazungumzaji wakuu ambapo aligusia kuwa kwa namna mambo yanavyokwenda haoni kama Katiba mpya itapatikana kabla ya 2030. Tukio hilo limetokea wakati wa mkutano huo unaoandaliwa na Tanzania Centre for Democracy (TCD), na kusababisha shughuli za mkutano kusitishwa kwa muda. Kufuatia tukio hilo, Mwenyekiti wa TCD, Dorothy Semu, ametangaza mapumziko mafupi ili kuruhusu hali kutulia na hatua zinazohitajika kuchukuliwa. Hadi sasa, taarifa zaidi kuhusu hali ya kiafya ya Jaji Warioba baada ya kuanguka kwake hazijawekwa wazi ingawa baada ya takriban dakika 10 Mzee Warioba alisimama na kwa usaidizi wa watu walio karibu naye waliondoka mkutanoni. Mkutano huo ulikuwa ukijadili hali ya kisiasa nchini pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa demokrasia na siasa nchini Tanzania. #ChawamataTV #10KFollowers #Asanteni #DarEsSalaam #Tanzania #Bongo #Habari #HabariLeo #BreakingNewsTZ #TanzaniaNews #BongoUpdates #TzUpdates #TzNews #BongoMedia #MediaTanzania #OnlineTV #TrendingTZ #tanzaniatrending

CHAWAMATA TV
CHAWAMATA TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Monday 07 September 2026 10:10:52 GMT
16130
470
27
35

Music

Download

Comments

jay_cob..angelin
Jay_cob. Angelin :
Nchi haijafikia mwisho kuwatumia hawa watu. Kweli hakuna watu wengine kufanya wanayoyafanya?
2026-09-07 12:25:47
5
daudisanga10000
Ds_family :
Kuna kitu kilimjia akakiangalia je ni nini tumuombee napia tumuombee Mungu atusaidie sisi wanadamu tunapita tu
2026-09-07 13:02:36
3
mokarachi4
mokarachi4 :
iyo maic ipo sawa kweli
2026-09-07 11:34:13
6
fozidy3
Mr Idafa :
Alisimama muda mreeefu saaaana Pole saaaana Jasiri mwongoza njia Uzee wako hakika utakumbukwa...
2026-09-07 11:16:38
2
bushirimagu
azora :
pole mzee wetu jaman unaipambania inchi yako japo kwa umri wako sasa na utumishi wako kwa umma huna cha kupoteza zaidi ya kutuhurumia
2026-09-07 10:56:21
2
brightchabu
bright chabu🦍 :
daah tayari.😥😥
2026-09-07 10:36:06
3
shariff.hasan
Shariff Hasan :
dunia inamuhukumu
2026-09-07 12:29:07
1
zombie.kid66
TERRY jr🏹🏹 :
kashachoka jaman pumziken
2026-09-07 11:05:19
0
hajihajivuaimw
Brohsjiv :
Awe pole. Apone haraka.
2026-09-07 17:15:30
0
chrisngao_2024
Ngao Chris 2024 🦁🦁🦁 :
hongereni askari wa Tz mpo makini na ulinzi
2026-09-07 11:51:57
1
emanueliwildauson
emanueliwildauson :
mze wa maana kabsa huyu
2026-09-07 14:12:30
0
matanga435
matanga :
mhm
2026-09-07 10:50:36
0
beuybet
Beuybet :
Sema Warioba tulitakiwa tuumpe ata Urais😔
2026-09-07 12:01:08
0
shafirumohamed
shafiru m,kashato :
mzee anaone kana kiafya hakuwa saw hata sauyiyake haitoki km tulivyo izoeeya mungu amuwekesawa afyayake
2026-09-07 13:13:45
0
ju_night24
Deo_datus 24 :
angalia vzr apo kuna kitu ame kiangalia mara ya kwanza aka endelea kuongea alivo angalia mara ya pili ndipo aka ishiwa nguvu ALLAH MJALIE MZEE WETU AWE SALAMA AMEEEN
2026-09-07 17:12:52
0
mustafanaida
Abuusalman :
akae na watoto wake umri umeshaenda achane na masuala yanayoleta presha
2026-09-07 14:47:44
0
rickyautospare759
Ricky auto spare parts 🔩🔧🔧 :
kipaza tayr washakitia
2026-09-07 12:53:39
0
user6294321628058
user6294321628058 :
Warioba pumzika!!!
2026-09-07 12:31:01
0
maumau.march.mwan
Maumau march Mwana wa adamu :
nimependa vile wamemuokoa
2026-09-07 10:31:56
0
user2443456104786
arbaab :
kamuona esrail huyo umeona alivyogeuka then kapoteza nguvu hapo hapo
2026-09-07 15:13:48
0
To see more videos from user @chawamata_tv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About