@rubabaimani: Kwenye sekta ya Kilimo na Ufugaji, bado kuna fursa nyingi ambazo watu wengi hawajaziona au hawajazichangamkia kwa wakati. Na wakati mwingine, fursa kubwa inaweza kuwa karibu yako kabisa. Tulipofika Manyoni, tulitembelea Mnada wa Mifugo wa Manyoni, ambako tulikutana na mjasiriamali aliyejitambulisha kama Mwalimu Nginga. Licha ya kuwa ni mwalimu wa sekondari, Mwalimu Nginga hakusubiri mshahara pekee. Aliamua kuchangamkia fursa ya kufuga na kuuza mbuzi—na leo anaendelea kujenga biashara yake kupitia ufugaji. 👉🏾 Je, ufugaji wa mbuzi unaweza kuwa biashara yenye faida? 👉🏾 Anaanzaje kama mfugaji mpya? 👉🏾 Anauza wapi na anapataje soko? 🎥 Tazama video hadi mwisho tujifunze kutoka kwa Mwalimu Nginga na kuona namna anavyotumia ufugaji kama fursa ya kuongeza kipato. Usisubiri fursa ikupite—ichangamkie mapema! #RubabaMedia #TanzaniaNaKilimo #Ufugaji #Mbuzi #UfugajiWaMbuzi
Imani Lubaba
Region: TZ
Monday 07 September 2026 14:02:30 GMT
Music
Download
Comments
There are no more comments for this video.
To see more videos from user @rubabaimani, please go to the Tikwm
homepage.