@focustvtz: Katika kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi kuelekea mbio za kitonga marathon, Askari huyu ameonyesha hamasa na uchangamfu wa kipekee wakati akishiriki mazoezi ya jogging, ikiwa ni maandalizi ya ushiriki na hamasa kwa wananchi kuelekea mbio za Kitonga Marathon zitakazofanyika Oktoba 31, 2026, katika Mlima Kitonga, Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa. Ushiriki huo umeonesha ushirikiano uliopo baina ya wananchi na vyombo vya usalama katika kuimarisha umoja na mshikamano katika jamii, pamoja na kuchochea juhudi za kuleta maendeleo katika jamii. #FocusTVTanzania