@jeremiahkisinza_: Ukisoma Vizuri 48 Laws Of Power, Utaanza Kuona Hivi Vitu... Kama Ukisoma Vizuri Na Kukielewa Kitabu Cha 48 LAWS OF POWER, Kuna Vitu Vingi Utaanza Kuviona Kwenye Maisha Kwa Namna Ya Tofauti Sana. Na Ukishaanza Kuviona Huwezi Acha Kuviona Tena... . Kuanzia Kwenye Maisha Ya Kila Siku, Movie, Siasa, Dini Na Kadhalika. Mfano, Niliposoma Sheria Ya 41 Inayosema: Avoid Stepping Into A Great Man’s Shoes. Sheria Inayomaanisha Epuka "Kutembelea Upepo" Au Kubaki Kwenye Kivuli Cha Watu Wakubwa, Hasa Kama Aidha Ni Wazazi Matajiri Au Maarufu n.k . Mwandishi Anasema Kama Unataka Kujenga Jina Lako, Hakikisha Haubaki Chini Ya Kivuli Cha Wazazi/Ndugu. Kivuli Cha Umaarufu/Utajiri Wao... Jenga Empire Yako Mwenyewe. (Kumbuka Haya Ni Mawazo Tu Ya Mwandishi. Tuendelee) Mifano Kwenye Maisha Yetu Ya Kila Siku Iko Mingi Sana, Nitakupa Baadhi . Kwenye Movie Ya CREED 1 Johnson, Mtoto Wa Creed, Alikataa Kutembelea Jina La Baba Yake Aliyekua World Champion Kwenye Boxing. Na Badala Yake Akataka Kujenga "His Own Legacy" Na Akafanikiwa Kujenga Jina Lake, Japo Jina La Baba Yake Lilimpa Attention Kubwa. . Mo Dewji Alichukua Biashara Kutoka Kwa Baba Yake, Lakini Amejenga Jina Lake Mwenyewe. . Aliko Dangote Babu Yake (Upande Wa Mama) Alikuwa Tajiri Na Mfanyabiashara Mkubwa Tu, Lakini Amejenga Jina Lake Mwenyewe. . Mifano Iko Mingi Sana... . Na Hii Ndio Faida Ya Kusoma Huku Una Reflect Ulichokifunza Kwenye Jamii Yako. Usisome Tu Kujaza Kichwa Na Ukakosa Kuona Namna Ambavyo Ulichosoma Kinaweza Kukusaidia Au Jinsi Kinavyoendelea Kwenye Jamii. Soma Kitabu, Elewa, Husianisha Na Maisha Yako Ya Kila Siku, Na Fanyia Kazi Kama Kuna Cha Kufanyia Kazi. . Narudia: Usisome Tu Kujaza Kichwa Na Ukakosa Kuona Namna Ambavyo Ulichosoma Kinaweza Kukusaidia Au Jinsi Kinavyoendelea Kwenye Jamii. Soma Kitabu, Elewa, Husianisha Na Maisha Yako Ya Kila Siku, Na Fanyia Kazi Kama Kuna Cha Kufanyia Kazi. . Umepata Kitu? . Wako Katika Ujenzi Wa Fikra 🧠📚 Jeremiah Kisinza Mwandishi Vitabu #jeremiahkisinza
Jeremiah Kisinza
Region: TZ
Tuesday 08 September 2026 07:13:09 GMT
Music
Download
Comments
Qiramy Hussein :
perfect🔥📌 Lkn hiki kitabu ni bei gan nataman kuwa nacho ila sijui bajet halisi
2026-09-08 11:27:55
1
Abbou :
Bro hao waliandika hawataki tuendelee ndo maana wanatulisha matango pori ndo maana familia nyingi sana za afrika ni masikini coz ya mtu mmoja mmoja kuwa tajiri au kujitengenezea utajiri mwenyewe na akipotea ndo basi tena ila wenzetu wana familia stron utasikia rich familly au familia/kingdom flan. Kama unaplan za kwako peke ako sawa ila kama tunaplan ya kizazi ad kizazi kisiteseke bas nikushirikiana na kuungana kutembea na mawazo ya waliofanikiwa katika familia kwa manuafaa ya pamoja…..
2026-09-08 12:42:42
10
el engineero :
kipo kilichoandikwa kiswahili?
2026-09-08 19:21:15
0
Rhoda Paul😊🤭 :
thanks,kitabu nakipataje
2026-09-09 04:44:15
0
Manka Mushi :
Kwenye vitu vya maana Kama hivi comments chacheee😂😂😂
2026-09-09 07:18:13
0
Jaramane :
Na iphone je
2026-09-08 17:02:32
0
Maji Taka :
Hii ni uongo bna 😂😂
2026-09-08 17:11:04
1
L :
ni mtazamo wako pia. we andika vitabu mwanetu ila haiimaanishi huwez toboa bila kupitia watu wakubwa.
2026-09-08 22:04:59
0
official msangu :
next time maliza kila kitu kwa display
ina kaa poa sana, ustupeleke kwa caption mkuu ni maoni tu 🙌
2026-09-08 13:11:50
0
Ginter Renatus :
unastairi mau yako🥰🥰🥰
2026-09-08 08:46:59
1
Jopesa :
😂😂😂
2026-09-09 08:23:57
0
Call me Icon4️⃣5️⃣.... :
🔥🔥🔥
2026-09-08 20:57:22
0
mr_planer♐ :
🔥🔥🔥
2026-09-08 09:03:27
0
Kijana Wa Leo :
🔥🔥
2026-09-09 16:26:02
0
To see more videos from user @jeremiahkisinza_, please go to the Tikwm
homepage.