@jambotv_: VIDEO: Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, ameitaka jamii na wanasiasa kutafakari kwa kina dhana ya mabadiliko ya katiba, akionya kuwa mchakato huo unapaswa kuheshimu historia ya nchi badala ya kujaribu kuunda nchi mpya au kunakili katiba za nje. Akizungumza Septemba 8, 2026, katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini unaofanyika mkoani Dar es Salaam, mwanasiasa huyo mkongwe amejibu hoja za viongozi wa upinzani kuhusu mabadiliko ya katiba huku akigusia uhusiano wa muungano na mustakabali wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU/SUK). Kuhusu hali ya kisiasa ya Zanzibar, Wasira ameeleza imani yake kuwa tofauti zilizopo katika kukamilisha na kuanza kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) zinaweza kutatuliwa na kuundwa kwa serikali madhubuti kwa ajili ya kuleta utulivu (stability), ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya nchi yoyote. Pamoja na matumaini hayo, Wasira alirusha "swali la kichokozi" kwa chama cha ACT Wazalendo akitaka ufafanuzi wa kisera kuhusu msimamo wa ACT Wazalendo unaodai "Zanzibar yenye mamlaka kamili". Amehoji maana halisi ya mamlaka hayo kamili kwa kusema kuwa kwa sasa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano na inayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inayoshughulikia takriban mambo yote ya Zanzibar, isipokuwa mambo machache. Ameonya kuwa kutofafanuliwa vizuri kwa dhana ya "mamlaka kamili" kunaleta mkanganyiko mkubwa kwa wananchi na kunaweza kuamsha migogoro hadi Tanzania Bara “Sasa unaposema Zanzibar yenye mamlaka kamili... inakuwa sehemu ya muungano au inakuwa sovereignty? Na kama inakuwa sovereignty, huo ndio mwisho wa United Republic of Tanzania au inakuwaje? Hili ni jambo kubwa ambalo nalo tusipolifanyia ufafanuzi linayumbisha watu,” amesema Wasira.
Jambo TV
Region: RO
Tuesday 08 September 2026 09:17:03 GMT
Music
Download
Comments
Mwakihongosi Measy :
Wasira is spitting fire live and direct…. Sasa hawa ndio wazee tunaowahitaji katika hili taifa..very sober mind for prosperity and progress..👏🏾👏🏾
2026-09-08 19:23:57
0
Abdul Hafidh :
sio Muda wakutawaliana huu tunataka mamlaka kamili ya Zanzibar
2026-09-08 10:49:32
5
FAHAD GENERAL TRADERS :
sawa leo umeuliza swali Zuri mzee wasira
2026-09-08 12:09:16
5
zanzibar :
zanzibar haiwez kufany chcht bila idhni ya bara
2026-09-08 10:48:10
2
Mtiga jr.....(Teamwork 💪🏼 :
kama Zanzibar wana katiba sisi Tanganyika mbona hatuna katiba
2026-09-08 20:24:17
0
MSHAMBA :
mhu haya
2026-09-08 13:27:24
1
Seif Kabelele :
OK
2026-09-08 17:21:27
0
Modey_mo :
mh
2026-09-08 12:17:26
0
Hawa Mohammed :
wewewee hatutaki mungano wenu
2026-09-08 13:09:27
0
MYRA COLLECTION TZ :
uyu mzee nikimsikiliza adi nachoka mm
2026-09-08 10:11:34
2
Abdul Mhina Mgosi :
Yaani we acha tu
2026-09-08 09:56:00
0
MEJJA MIZOZO 🇹🇿 :
mku othuman katulia
2026-09-08 14:53:58
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm
homepage.