@valentina_thhomas30: Moja ya vitu vinavyotufanya tuweze kuendelea, hata pale maisha yanapokuwa mazito, ni kutambua na kuthamini watu wanaosimama nasi. Wale wanaotuamini hata tunapojishuku. Wanaotushika tunapoanguka. Wanaotuombe, Wanaojitoa kwa ajili yetu bila kutafuta sifa. Na wale wanaobaki, hata wakati si rahisi kubaki. Wakati mwingine hatuna uwezo wa kuwalipa kwa yote waliyotufanyia. Hatuna maneno makubwa ya kutosha, wala zawadi inayoweza kufanana na upendo, muda na uwepo wao. Lakini tunaweza kusema asante. Na pengine, shukrani ni kitu kidogo zaidi tunachoweza kuwapa watu ambao wametupa mengi sana. Usisubiri kuwapoteza ndipo utambue thamani yao. #beyondhealing #fyp #viral #tanzaniantiktok🇹🇿 #kenyantiktok🇰🇪