@jambotv_: VIDEO: Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini wa Septemba 8, 2026, umegeuka uwanja wa mnyukano mkali wa hoja baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), Profesa Elgidius Ichumbaki, kukishutumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendeshwa na "dude" lisilojulikana, huku Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, akijibu kwa kuwataka wasomi kuacha kulinganisha hoja zao na "mambo ya mitandao ya kijamii". Profesa Ichumbaki amefunguka kumweleza mzee Wasira pamoja na viongozi wengine wa CCM kuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao wa kikatiba, kisheria, na kijamii wa kuisimamia serikali ipasavyo. Profesa Ichumbaki amekwenda mbali zaidi na kuhoji kama kweli CCM inayo mamlaka kamili ya maamuzi nchini, akidai kuwa kuna nguvu nyingine ya siri inayoratibu mambo. Aidha, amegusia ahadi ya CCM ya kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya ndani ya siku 100 za kwanza za uongozi wa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, akidai kuwa wanachama wanaosimama kudai katiba hiyo, na wengine kutetea haki nyingine za wananchi wamekuwa ‘wakiadhibiwa’ na kufukuzwa uanachama wa CCM. Akimjibu Ichumbaki, Wasira, amepinga vikali madai kuwa watu wanaoongea kwa niaba ya wananchi wanashughulikiwa akisema, “Yeye anasema mtu akisema kwa niaba ya mambo wanayotaka wananchi anashughulikiwa. Sio kweli. Na wewe kwa kuwa ni msomi, na wasomi wana sifa moja kubwa ya kufanya utafiti. Utafiti ni sehemu muhimu ya usomi. Usipotafiti utasema chochote tu. Utakuwa kama mitandao ya kijamii ambayo haina control”. Wasira amekitetea chama chake akisema kuwa wanachama na viongozi wa CCM nao ni sehemu ya wananchi na sio malaika, hivyo nao wana haki na uwezo wa kutoa maoni yao huru.
Jambo TV
Region: TZ
Tuesday 08 September 2026 14:40:17 GMT
Music
Download
Comments
~Eli :
kweli sometimes kipara ni busara wakuu
2026-09-08 16:35:56
141
user3852971019163 :
kwel kabsa brother umeongea point sana Mungu akulinde
2026-09-08 15:33:39
437
flavykiwale7 :
zee la ovyo ili
2026-09-08 15:31:30
219
God is a provider :
give the country to young people 🥰🥰🥰
2026-09-08 20:41:13
0
The middle :
mzee mwema kabaki 1 tu tz
2026-09-08 17:41:25
105
Masiara :
Let's put Tanzania in God's hand.
2026-09-08 18:16:41
0
Bamnyong'ode :
Ila Wasira has point, lets be honest
2026-09-08 16:35:49
32
SALIM MPINGA 26 :
Mungu ikikupendeza bc fanya na hiki najua kwako ni kidogo ila kwetu ni kikubwa..🥰🥰
2026-09-08 15:45:53
88
NEWTON_JR :
very fact
god bless you
2026-09-08 17:09:11
1
bin issa ktchen dish :
kiufupi CCM hatuitaki🙌
2026-09-08 17:54:58
38
abdalahmsangi111 :
ukweli unauma aisee
2026-09-08 15:21:23
110
Treasure :
mhhhh short on target 🎯 irtakiwa apaa
2026-09-08 19:45:32
0
youngmado :
yani October 29 imeathiri mchakato wa katiba lakini haikuathiri ushindi wa 98%
2026-09-08 17:20:51
54
Grace :
Ukweli usemwa🙏🙏🙏🙏🙏
2026-09-08 15:48:33
28
king sam :
wasira mhhh
2026-09-08 19:22:09
0
Godfrey Gumie :
kaka umetisha umeongea ukwel
2026-09-08 15:32:26
140
Mussa :
mzee hajajibu swali
2026-09-08 15:43:23
46
rapaitotaikomolle :
kaka hongera umepeleka ukweli
2026-09-08 16:35:58
36
Halima kisuda :
Kaka uko vizuri Sana na ukweli unauma
2026-09-08 15:37:34
39
Msafiri Mgavilenzi :
eeee munguu tenda jambo kwa huyuu mzeee ikikupendeza mungu baba
2026-09-08 15:58:13
54
alito d ommy💵🎧 :
mbon me cjamuelew huyu mzee
2026-09-08 16:54:09
17
Goodlucky JS :
Dua za watanzania😂😂🙌🏿
2026-09-08 16:41:23
12
user CanRap :
Ukweli mchunguuu 😅
2026-09-08 15:58:02
13
mark magari :
uo niukweli mtupu kaka
2026-09-08 15:39:43
19
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm
homepage.