@mansamussaxivcom: Nimetishiwa kifo na kuambiwa watanipoteza kwa sababu tu nimewaonesha Watanzania hesabu za pesa. Sasa jiulize… nani anafaidika Watanzania wakiendelea kuwa hawajui hizi hesabu? Mimi sitaacha kuwaelimisha. Sasa ngoja nikuoneshe kwanini mtu anayeanza ku-invest akiwa na miaka 20 anaweza kuwa na zaidi ya TZS 400M kuliko anayeanza akiwa na 30. Tuchukulie: • Una-invest TZS 100,000/month • Average return: 10% kwa mwaka • Average monthly return: 10% ÷ 12 = 0.83% • Investment inakua kwa compound growth mpaka miaka 60. MTU A: Anaanza miaka 20 40 years × 12 = 480 months 100,000 × 480 = TZS 48M alizoweka mwenyewe. Kwa average growth ya 10% annually: 👉 Final value ≈ TZS 632.4M MTU B: Anaanza miaka 30 30 years × 12 = 360 months 100,000 × 360 = TZS 36M alizoweka mwenyewe. Kwa growth hiyo hiyo: 👉 Final value ≈ TZS 226M Sasa angalia: 632.4M − 226M = TZS 406.4M Mtu aliyeanza miaka 20 ana zaidi ya TZS 406M MORE. Lakini aliweka kutoka mfukoni: 48M − 36M = TZS 12M zaidi tu. Yaani ameongeza contribution yake kwa 12M tu, lakini miaka 10 ya ziada imempa advantage ya zaidi ya 406M. Hiyo ndiyo nguvu ya TIME + COMPOUND GROWTH. Growth yako inaanza ku-generate growth nyingine. Kwa hiyo ukiwa na miaka 20 usiseme: “Pesa yangu ni ndogo, nitasubiri miaka 30.” Hata kama ni 20K, 50K au 100K kwa mwezi — ANZA. Kwenye investing, muda unaweza kuwa na thamani kubwa kuliko amount unayoanza nayo. Kumbuka: 10% ni assumption ya mfano, si guaranteed return. 📕 Siri 69 za Kupata Pesa — madini yote yapo humo. Nenda kwenye bio yangu chap ukakichukue kabla havijaisha. Peace ✌🏾
Mussa Baba’s
Region: TZ
Tuesday 08 September 2026 15:32:41 GMT
Music
Download
Comments
Lickson jeremia 🇹🇿🇰🇪 :
siwezi kuwekeza huo ujinga miaka yote hiyo wakati kulima ni mieezi 3 tu
2026-09-08 18:40:48
25
Olaedo🍀 :
upo sahihi lakini tuwaambie vijana UTT ni kwa ajili ya kustaafu sio kujikwamua kiuchumi ukiwa kijana, mtu ambae anajitafuta kupata mtaji saizi usimuaminishe kua akiweka UTT atapata huo mtaji kwa muda anao uhitaji
2026-09-09 08:14:17
3
martin Davidy :
haiwezekan kaka
2026-09-08 17:24:02
5
Joseph Sembuli :
mimi nisie jua UTT nini na park wapi
2026-09-08 17:31:51
8
Collins :
on point
2026-09-08 18:30:59
3
MR.HUSBAND :
STOP UTT kijana hizo hesabu ni za kulinda pesa sio kuongeza pesa
2026-09-09 05:40:56
2
❦𝓳𝓸𝓳𝓸 🦋✨ :
tuelekeze jmn
2026-09-08 23:38:47
1
HARDWARE POINT DAR :
Ukiweka milioni 100 UTT, faida ya mwaka ni 12% hadi 15% (milioni 12 hadi 15), lakini ukitoa mfumuko wa bei wa takriban 5% (milioni 5), faida halisi inayobaki ni ndogo sana, ilhali ukiwekeza hata milioni 30 kwenye biashara na ukajiajiri unaweza kurudisha nusu ya mtaji huo ndani ya mwaka mmoja, hivyo UTT si sehemu ya kufanyia biashara au kutengeneza utajiri wa haraka bali ni sehemu ya kulinda usalama wa fedha zako na kuzuia zisipoteze thamani.
2026-09-08 21:22:19
6
perlot☃️ :
Great info but the shirtless setup makes it awkward to watch in public
2026-09-08 17:50:50
4
stellafaraja607 :
UTT ni ya kuanza sasa sio baadaye
2026-09-09 01:11:18
1
L A L U U :
Akutishie nani bhna embu tuachee 😂
2026-09-09 06:02:44
2
SAB TECHNOLOGIES :
kila mtu atumie njia zake kuwa tajiri😂
2026-09-08 19:45:52
4
urassag :
mimi naushahidi nilinunua za 35000nikiwa na mimba yamwanangu 2006juzi niliishiwa nikaenda pale kitega uchumi nikauza nikapewa laki7nachenji jiulize ningeweka million 3na nusu jeeee?
2026-09-08 18:07:39
4
Fravian33 :
UTT Ndo nini
2026-09-08 18:13:53
2
henry john :
tufanye kaz 😁😁😁😁usituchoshe bana😁
2026-09-08 17:26:01
5
LauTronics :
UTT ni kama safari ya Natumaini ya maisha na Kifo. huwezi weka laki kwa mwezi kwa MIAKA 30. imagine unamiaka 20+30= 50. ni wanaume wangapi wanakufa kabla ya kufikisha hio MIAKA 50.
2026-09-09 08:50:17
0
...Engineer💫 :
kaka acha uongo mm UTT Nimeanza mapema na sijaona chochote
2026-09-08 20:03:39
1
Engineer by Nature :
Hadithi za matikiti mnazileta kwenye mambo serious
2026-09-08 17:42:44
9
Erick Alisen :
Sehemu ya kutoa iyo laki moja shida sio kutunza bro
2026-09-08 18:01:44
3
Tone skills :
mil 400 kwa miaka 30 ijayo ni ndogo
2026-09-08 21:28:53
0
CAIN TRONICS :
aah kwanza hii ni secta ya serikal au private maana siwezi riski ufala
2026-09-09 05:59:01
1
Joseph Osward :
dah nashukuru Kwa kujua kaka
2026-09-09 04:55:55
1
ESSENTIAL TECHNOLOGY POINT :
umetisha kijana
2026-09-08 19:56:50
1
To see more videos from user @mansamussaxivcom, please go to the Tikwm
homepage.