@icon.communication: Naibu Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Dkt. Doto Biteko amezungumza na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Alexander Mnyeti na Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Martine Shigela wakati wa makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita na amewataka wafanye kazi kwa bidii katika maeneo ambayo wameaminiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita,uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Geita ambao ulihudhuriwa na wakuu wa wilaya, wenyeviti wa halmashauri, wakuu wa taasisi, watumishi wa taasisi binafsi na za serikali.