@katorotv: Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Matiko Chacha, amesimulia kisa cha mwananchi aliyemtaja kwa jina la Sophia, ambaye alikuwa akimtumia ujumbe mfupi wa simu wa kumtongoza, licha ya kuonywa mara kadhaa kuacha kufanya hivyo. Chacha amesema mwanadada huyo aliendelea kumtumia ujumbe huo, hali iliyomlazimu kuchukua hatua kwa kulifikisha suala hilo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora (RPC), hatua ambayo amesema ilimfanya Sophia kuacha kabisa kumtumia ujumbe. Amesema kabla ya kufikia hatua ya kutoa taarifa kwa RPC, alitumia njia mbalimbali za kumfikia mwanadada huyo kupitia wajumbe waliokwenda kumuonya na kumtaka kuacha kumtumia ujumbe wa aina hiyo, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda. Chacha amesimulia kisa hicho Septemba 7, 2026, wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi kati yake na Mkuu wa Mkoa mpya wa Tabora, Beno Malisa. Katika hafla hiyo, Chacha amekabidhi rasmi majukumu ya uongozi wa Mkoa wa Tabora kwa Mkuu wa Mkoa mpya, Beno Malisa.

KATORO TV
KATORO TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 09 September 2026 08:38:36 GMT
103153
2877
327
92

Music

Download

Comments

moreenelia0
momo :
mbona sisi mkitutongoza hua hatu washtaki namnakuaga wasumbufu kama nini
2026-09-09 11:56:58
28
husnaramadhan456
husnaramadhan456 :
mm sasa hivi mtu akinitongoza naenda polisi akamatwee😂😂😂😂
2026-09-09 12:13:57
17
user85709457406946
Ummu Mayrah💝 :
Sofia sofiaa😄😄 et usitake ntumie nguvu😄😝😝
2026-09-09 13:18:35
0
peterombeni253
a man of the people 0123 :
weee nae
2026-09-09 13:57:23
0
rose.samwel23
Rose Samwel :
Asa jaman mtu asiseme hisiazake acha uchoyo mkuu
2026-09-09 10:55:24
12
jelemia812
Jelemia :
mbona jpm alitongozwa hadharani na hakufungua kesi😂😂😂 anyway yanga bingwa
2026-09-09 10:32:27
14
el844359
Qu💞💞💤 :
kwani namba yako aliipataje kama hujamfata wewe na kumtongoza
2026-09-09 12:29:44
9
chrismnzava1
Chrismnzava :
hio Ni secret issue
2026-09-09 12:04:03
0
ashjklalakaaaaa1234
agustina ngatunga :
sophia ana haki jmn mbna ivo
2026-09-09 11:22:25
1
paulkahena
paulkahena :
siyo zambi
2026-09-09 10:39:18
0
agnessangawe13
sangawe :
YAANI UMEWAITA WATU KUFANYA MKUTANO NA KUWAPOTEZEA MUDA WAO KISA KUTONGOZWA?? KUTONGOZWA NA KUTONGOZA NI JAMBO LA KAWAIDA SANA??
2026-09-09 11:47:31
7
yusra6981
yusra :
Sophia Hana kosa mungu happend umuweke M2 hadharani
2026-09-09 11:22:52
13
michaellpeterpete
BABA G :
si ungemblock kulikua na haja gani ya kumshitaki
2026-09-09 14:28:32
6
operatorimmah
operator :
unajua nacheka kwann???? 🤣🤣🤣🤣🤣 haya n maajabu🙌🙌🙌
2026-09-09 16:53:16
1
bernadetadeograti1
Bernadeta Deogratias :
Kama kumupenda mtu nikosa bas MUNGU atusamehe Dunia nzima
2026-09-09 11:12:18
6
maganda88_tz
DR. RAMA🧑‍⚕️ :
na wazeee wanetoamimacho kusikiliza nchi yangu inaangamia kwa kukosa maarifa
2026-09-09 16:01:46
2
sj27876
SJ🌹🌹 :
mapenzi ni hisia
2026-09-09 13:46:00
3
roseharun8
Rose harun :
mmhhhhh
2026-09-09 09:35:14
2
daudi.samweli8
Daudi Samweli :
hana kosa dada wa watu kwa sababu na yeye ana moyo wa kupenda kwa sababu nayeye kaumbiwa moyo wenye matamanio usivuje hisia zake mheshiwa
2026-09-09 13:35:38
3
showalex830
showalex :
HILO SIO KOSA UNGEMBLOKU TU MHESHIMIWA MSAMEHE TU UTAPTA BARAKA KWA MUNGU
2026-09-09 13:37:35
2
user6131212566185
aggy's fashion :
ila kasema hisia zake jamani wanawake nao tunahisia jamani😊
2026-09-09 14:14:15
2
user481945269881
user481945269881 :
Kama amupendi mbona unacheka
2026-09-09 12:45:44
1
fatuma4957
FATUMA :
tanzania kuna sehemu haipo sawa
2026-09-09 13:38:26
1
aloyzsumaye
Aloyce Sumaye :
ukipendwa pendeka mkuu
2026-09-09 14:06:43
1
erca2692
Erca🦋🦋 :
Kwahy cku izi kumpenda mtu kosa😂😂
2026-09-09 13:24:51
1
To see more videos from user @katorotv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About