@wasafifm: Hata Dereva Mwenyewe Haamini Kama Ametoka Salama Baada Ya Ajali Hii Ya Kutisha. Kwa Mujibu Wa Fox News; Dereva wa mashindano Manuel Gil del Real amenusurika Kifo kwenye ajali mbaya iliyohusisha gari lake aina ya Porsche baada ya kushindwa Kuzuia breki akiwa kwenye Speed Ya Ajabu huko California. Gari hilo lilitoka nje ya barabara na kupinduka mara kadhaa katika tukio lililowaacha wengi wakiwa na hofu. Licha ya kupata majeraha na kukimbizwa hospitalini kwa uchunguzi na matibabu, Manuel amethibitishwa kuwa yupo salama. Kwa bahati nzuri, hakuna mtu mwingine aliyejeruhiwa katika ajali hiyo Iliyotokea Sept 5, 2026. 🎥: Fox News #wasafifm #wasafimedia #WNews