@chawamata_tv: VIDEO: Dereva wa lori anayefahamika kwa jina la Feisal Jabir, mwenye umri unaokadiriwa kuwa kati ya miaka 35 na 40, amefariki dunia baada ya kudaiwa kupigwa risasi na mlinzi wa kituo cha mafuta kilichopo Kihonda Viwandani, Manispaa ya Morogoro. Kwa mujibu wa mashuhuda, marehemu alikuwa amepaki lori katika kituo hicho na kwenda msikitini kuswali. Baada ya kurejea, kulitokea malumbano yanayodaiwa kuhusiana na namna lori lilivyokuwa limepaki. Inadaiwa kuwa wakati dereva akiwa ndani ya lori, mlinzi alifyatua risasi na kumpiga, huku lori hilo baadaye likipoteza mwelekeo na kugonga magari mengine. Msaidizi wa dereva huyo amesimulia kuwa alisikia ghafla kioo cha gari kikivunjika, kabla ya kubaini kuwa dereva alikuwa amepigwa risasi. Kaimu Afisa Habari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Scolastica Ndunga, amethibitisha kuwa hospitali imepokea mwili wa marehemu na kueleza kuwa ulikuwa na jeraha katika eneo la kichwa. #ChawamataTV #10KFollowers #Asanteni #DarEsSalaam #Tanzania #Bongo #Habari #HabariLeo #BreakingNewsTZ #TanzaniaNews #BongoUpdates #TzUpdates #TzNews #BongoMedia #MediaTanzania #OnlineTV #TrendingTZ #tanzaniatrending #Asanteni #tanzaniatrending #tanzaniatrending_habari #tanzaniatrendingsong #mediatanzania #tanzaniatrendingvideos #tanzaniatrendingstory #TanzaniaTre #madeintanzania🇹🇿 #madeintanzan #madeintanzania #SupportLocal #madeintanzaniat #roadto100followersontwitch #madeintanzaniawith #chawamata_tv #viraltz

CHAWAMATA TV
CHAWAMATA TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 09 September 2026 13:24:50 GMT
103984
4828
267
190

Music

Download

Comments

user7035851838335
smart boy 06 :
mashaaallah kafa katoka msikitini bora ningekua nimekufa mm 😭😭😭
2026-09-09 16:26:38
90
emanuelyandrewsondaafrik
its kenzo officialy Tz :
huyu mlinzi watuachiee na ss madereva tuish naee🙏
2026-09-09 14:55:13
49
calvin.boy57
Calvin boy :
kampuni ya ulinzi ni ya kufungiwa
2026-09-09 14:29:54
45
president.wake
muhboe💕 :
sio fear
2026-09-09 20:11:30
0
user9707435332021
immani :
kwanni sisi madereva tunaonewa sanaa katika sekita zote
2026-09-09 14:14:53
36
ramadhani.amir2
Ramadhani Amir :
feisali amekufa shahidi na amekufa akitoka kuongea na mungu wake kaitwa na kaitika mungu ampokee
2026-09-09 16:38:09
82
new.kivuruge.boy
new, KIVURUGE >>> BOY :
duh R.I.P
2026-09-09 20:02:06
0
its_gvan_geo
그반❤️‍🩹🦅 :
Eeeh Mungu nilindie yule kijana 🥹🙏..na madereva wenzie wote.
2026-09-09 16:26:59
32
sir.sembeta
Mr Julius :
ndio maana kazi ya security sipendagi yanii mtumwa anamuua mtaftaji
2026-09-09 16:37:37
15
user556692876688
thamairat :
pepon moja kwa moja kwa uwezo wa mungu inshaallah ♥️
2026-09-09 16:47:29
40
preciousmoraa675
precious :
makosa niyadereva
2026-09-09 17:27:08
3
ramadhanimanyagal
Ramadhani Manyagala :
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi
2026-09-09 17:55:18
7
user5516103007398
jumaaMartin14 :
innalillah wa inna ilayh raju-uun Allah aiweke roho ya marehem mahala pema peponi insha Allah🤲🤲
2026-09-09 15:06:20
23
aww107ajs
aww107ajs :
Mlinzi anapata wapi mamlaka ya kumiliki bunduki na amechukuliwa hatua gan
2026-09-09 16:32:53
3
mrplantz256
Geita finest🛣️ :
hapa sijaelewa dereva amefariki au
2026-09-09 14:35:16
1
hajrashekinyashi1
hajrashekinyashi :
mashalah kafa na udhu wake
2026-09-09 20:32:40
1
225.janeth
225 Janeth :
Bora alikua ametoka kuswali ila inauma mke wake anajua mwanaume yupo kazn analetewa maiti dah😭
2026-09-09 16:25:10
9
paluhengo3
Ezzy 7 :
mh jamani nchi yangu sasa mambo nimengi sanaaa! mungu tusaidie
2026-09-09 14:55:41
8
user2133014144950
@ummy ima :
kazi kiwadhulumu watoto maskin jamani mtu kenda kutafuta riski hee jamani hii kuuwa imekua kama kula kilasiku hee jamani washamdhulumu roho yake
2026-09-09 20:47:08
1
munisi829
munisi :
kwani police walikuwepo jaman mpaka wao ndio wagoe taarifa hii serikali ya Tanzania na sheria zake zikiongozwa na katiba 😎😎
2026-09-09 16:49:22
2
khalfan12031
khalfan1203 :
innalillah wa inna ilayh raju-uun🤲🤲🤲
2026-09-09 16:46:38
2
adam44.c
adamMathias :
kwani mlinzi yeye anasemaje
2026-09-09 19:33:26
1
hadija_jma
NANA :
saahzi kashapokewa na malaika wema pamoja na mtume na shangwe nyingi inauma kwa familia lkn kafa shahidi Allah amrehem🥺🥺
2026-09-09 16:50:39
4
user6594018617143
user6594018617143 :
haya maisha watu wanapenda kujiamulia mambo
2026-09-09 17:14:18
2
godwinmikidadi
ISUZU FAN TANZANIA 🇹🇿 :
mlinzi Yuko wapi baada ya tukio
2026-09-09 16:29:16
1
To see more videos from user @chawamata_tv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About