@greenwavesmedia: Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imefanikiwa kukamata **mzigo wa dawa na vifaa tiba visivyosajiliwa wenye thamani ya takribani Sh. milioni 310** katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari leo **Septemba 9, 2026**, katika Ofisi za TMDA Kanda ya Mashariki, Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, **Adam Fimbo**, amesema mzigo huo ulikamatwa kupitia operesheni maalumu zilizowezeshwa na wakaguzi wa mamlaka hiyo katika viwanja vya ndege na maeneo mengine. Kwa mujibu wa Fimbo, mzigo huo ulikuwa na **mabegi takribani 20** yaliyojaa dawa na vifaa tiba mbalimbali, huku uchunguzi ukibaini kuwa **hakukuwa na dawa hata moja iliyokuwa imesajiliwa Tanzania**. Amesema baadhi ya dawa hizo zinaweza kuwa na madhara makubwa kwa watumiaji, wakiwemo **wanawake wajawazito**, huku dawa nyingine zikihusishwa na matibabu ya saratani na moja ikiwa na thamani ya takribani **Sh. milioni 7**. Fimbo amesema TMDA imeimarisha mbinu za udhibiti na kuweka mitego katika maeneo muhimu ili kuzuia dawa **bandia, duni na zisizosajiliwa** kuingia nchini. Ameeleza kuwa kiwango cha dawa bandia nchini kinakadiriwa kuwa **chini ya asilimia 1**, huku dawa duni zikiwa **chini ya asilimia 2**, na kusisitiza kuwa mamlaka itaendelea kuchukua hatua dhidi ya wanaojihusisha na uingizaji na usambazaji wa dawa zisizo salama. **“Hii ni sehemu ya udhibiti na majukumu yetu ya kila siku ya kuhakikisha dawa zisizosajiliwa haziingii Tanzania,”** amesema Fimbo. #GreenWavesMedia #TMDA #BreakingNews #Dawa #Tanzania

GREEN WAVES MEDIA
GREEN WAVES MEDIA
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 09 September 2026 14:25:35 GMT
14155
188
8
148

Music

Download

Comments

user._000123123
user :
tufafanunulie nn dawa feki sasa kama dawa haijasajiliwa kwenu ndo feki
2026-09-09 22:44:47
4
zenombele
mbunge2030 :
semeni hazina vibali... basi mwambieni alipie
2026-09-10 05:31:59
2
emmagmayemba
Emmanuel Mayemba :
kuna wagonjwa watakosa huduma
2026-09-10 01:23:02
1
million.mara
million Mara :
Binaadam tumefikia pahala pesa imekuwa ibada kuliko uhai wa mwanadam
2026-09-10 00:01:59
1
tuktane_
Karibu kwetu :
Sad
2026-09-09 19:45:08
0
odindo40
McOdindo :
DUH KUNA WATU WANAPATA HASARA.TUMUOGOPE SANA MUNGU
2026-09-09 16:42:57
0
user32851183793
sonda :
utaratibu gani tuutumie ili dawa zifike kwa wagonjwa wetu, bei ziko juu sana
2026-09-10 04:30:57
0
user._000123123
user :
mm siamini kama dawa zote ni feki nyinyi unataka watu maalum waingize kama feki zishtakini izo kampuni zilizotengetenezwa
2026-09-09 22:46:58
1
To see more videos from user @greenwavesmedia, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About