@jambotv_: VIDEO: Katika muendelezo wa maswali ya dodoso kwa shahidi wa nne wa upande wa utetezi katika shauri la uhaini linalomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Jonas Rupia, leo Septemba 9, 2026, amekutana na maswali ya kina kutoka kwa mawakili wa Serikali, yaliyolenga zaidi ushahidi alioutoa mahakamani. Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassor Katuga, alianza kwa kumuuliza Brenda kuhusu taarifa aliyoitoa kwamba Lissu alitaka kupewa sumu akiwa gerezani. Brenda alikiri kuwa hakutoa taarifa polisi kabla ya kuchapisha taarifa hiyo. Alipoulizwa kama anajua kuwa kutoa taarifa za jinai bila uhakika kunaweza kuwa kosa, alisema hajui, huku akikiri kuwa anafahamu sheria za makosa ya mtandao zinahusu utoaji wa taarifa zisizo na uhakika. Alipoulizwa kama katika uchunguzi wake alifanikiwa kumpata mtu aliyedaiwa kutoa taarifa kuhusu mpango wa kumpa Lissu sumu, Brenda alisema hakumpata. Hata hivyo, alisisitiza kuwa taarifa hiyo haikuwa ya uongo baada ya kufanya uchunguzi na kuzungumza na aliyempa taarifa.
Jambo TV
Region: TZ
Wednesday 09 September 2026 17:56:20 GMT
Music
Download
Comments
makemba03 :
maswali rahisi sana
2026-09-09 18:40:20
0
Usa-river Bc Biulding Constrcn :
Brenda mm ni mwanaume naomba unioe.
2026-09-09 20:57:30
0
mohamed mshola :
😂😂😂
2026-09-09 18:41:18
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm
homepage.