@jamiivoice_: HABARI: Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Peter Mwasalyanda, amesema ushiriki wa wadau wote ni muhimu katika kudhibiti matukio ya kihalifu yanayofanyika kupitia huduma za simu na intaneti. Mwasalyanda ameyasema hayo Septemba 7, 2026, wilayani Kilombero, mjini Ifakara, katika mkutano na wadau wa mawasiliano, wakiwemo kampuni za simu, viongozi wa Serikali, madiwani pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Amesema mafanikio katika juhudi za kudhibiti uhalifu unaofanyika kupitia mitandao yanategemea ushirikiano wa kila mdau katika nafasi yake, huku akisisitiza kuwa TCRA itaendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wote. Katika mkutano huo, viongozi na wananchi wa Ifakara wameelezwa umuhimu wa kushiriki katika kupambana na utapeli wa mitandaoni, hususan kwa kutoruhusu laini zao za simu kutumiwa na watu wengine. Mamlaka hiyo imeeleza kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakiruhusu watu wengine kusajili laini kwa kutumia taarifa zao kwa malipo madogo, kisha laini hizo kutumika katika vitendo vya utapeli. Wananchi wamekumbushwa kuhakiki laini zao za simu kwa kutumia *106#, kuripoti namba zinazotumika kufanya utapeli kwa kutuma ujumbe mfupi wenye namba ya tapeli kwenda 15040 bila malipo, pamoja na kutoa taarifa mara moja pindi simu inapopotea au kuibiwa. Aidha, wameonywa kutotoa ushirikiano kwa mtu anayejitambulisha kuwa mtoa huduma wa kampuni ya simu bila kuthibitisha, huku wakikumbushwa kuwa huduma za kampuni za simu zinapaswa kuthibitishwa kupitia namba 100; simu kutoka namba nyingine zinazodai kutoa huduma zinapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari.

Jamii Voice
Jamii Voice
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 09 September 2026 18:14:05 GMT
40397
690
8
42

Music

Download

Comments

salama.khalifa8
Salama Khalifa :
hakuna mzazi anaye msajilia mwanae ahusike na uhalifu mzaz atakuwa hajui mambo anayofanya mwanae
2026-09-10 11:19:24
5
siware.famiryy
Siware famiryy :
hakuna mzazi mwenye ujinga wanamna hiyo tuwasidie tuu!! hao watoto tupo WAKATI WA mwisho mungu atusaidie so kosa la waziza hapana
2026-09-11 13:23:24
0
davies_autfit1
Davies_outfit 🔥 :
si wanataka wawasaidie kulipa deni
2026-09-11 21:26:37
0
user317163461059
NABII SDK :
duuuu
2026-09-11 04:43:13
0
uheri52
Uheri :
waifakara n matapeli sana mm niliolewa na mtu wa ifakara yaan n msanii tapeli kama sio baba au mume isee nilichoka
2026-09-11 20:22:37
0
afrika.halisi1
Afrika Halisi :
Kutoka Tabata Mabibo Manzese Ubungo wakaamia Ifakara kwao baada ya kupewa Training na Wanigeria Sasa hata ukitapeliwa bongo upelelezi utaonesha mwizi yupo Ifakara
2026-09-10 16:16:04
0
kinguhamis
kingu hamis :
kweli mku wangu .tena kama hivi vitoto vya 2000
2026-09-09 18:40:42
0
chicharito1555
the don :
Kuna kitu nyie hamjuwi mawa kala wale WA mtaani ndio chanzo
2026-09-12 07:47:42
0
To see more videos from user @jamiivoice_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About