@wasafifm: Makamu wa Rais wa Bank of America, Erin Piacenti, mwenye umri wa miaka 32, ameripotiwa kufariki dunia jana Agosti 31, 2026 baada ya kuchomwa visu katika shambulio la ghafla huko Times Square, New York City, Nchini Marekani. Shambulio hilo la visu lilitokea mchana wa Jumatatu, Agosti 31, 2026, eneo la Times Square. Mwanamke mwenye umri wa miaka 49, aliyetambulika kama Pamela Cisneros, aliripotiwa kumshambulia Piacenti pamoja na mtu mwingine mwenye umri wa miaka 68 kwa kutumia visu. Polisi walimpiga risasi mshambuliaji huyo baada ya Kushindwa Kumtuliza kwa kutumia kifaa cha kumpa mshtuko wa umeme (Taser). Bank of America ilitoa taarifa ya kusikitishwa na kifo cha mfanyakazi wao, ambaye alikuwa akihudumu kama Makamu wa Rais wa Uteuzi wa Biashara na Migogoro (Vice President of Business Selection and Conflicts). Kifo cha Piacenti kimezua masikitiko kufuatia tukio hilo la ghafla lililotokea katika moja ya maeneo yenye shughuli nyingi jijini New York. #WNews #wasafifm #wasafimedia

WasafiMedia
WasafiMedia
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 10 September 2026 04:40:48 GMT
2230
24
0
0

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @wasafifm, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About