@shebyranco: Ukweli kuhusu video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha moto ukilipuka kutoka ndani ya kaburi umezidi kuwekwa wazi. Tukio hilo lililotokea katika makaburi ya Seyid Allavi eneo la Kirkuk nchini Iraq, lilizua taharuki kubwa miongoni mwa wananchi walioshuhudia na kuhisi kuwa huenda ilikuwa ni adhabu ya kaburini kama inavyoelezwa katika mafundisho ya dini. ​Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na kikosi maalum cha polisi na usalama wa raia nchini Iraq umebaini kuwa moto huo haukuwa wa kimuujiza wala adhabu ya kiimani. Imeelezwa kuwa moto huo uliwashwa kwa makusudi kwa kutumia kuni na mrundikano wa taka na vifusi vilivyokuwa pembezoni mwa eneo hilo, na sio ndani ya kaburi la mtu aliyezikwa. Vijana kadhaa wanatuhumiwa kuhusika na kitendo hicho ili kuzua taharuki na kujipatia umaarufu (engagement) kwenye mitandao ya kijamii. Video hii imepostiwa kwa madhumuni ya kutoa habari na kuwasilisha taarifa pekee. Sisi si wamiliki wa maudhui haya. Hata hivyo, mmiliki anaweza kuwasiliana nasi kwa ajili ya umiliki (credit) au kuondolewa kwa video hii. bbmtvtz haiungi mkono, haichochei, wala haishawishi ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa aina yoyote, ukatili, au tabia yoyote yenye madhara inayoonekana kwenye video hii. Lengo la bbmtvtz katika kushiriki video hii ni kuuhabarisha umma na kudumisha uwazi kama chanzo cha habari kinachoaminika.

shebyranco
shebyranco
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 10 September 2026 12:01:11 GMT
2612
142
6
15

Music

Download

Comments

user3319219388178
khadija :
Allah Aqbr
2026-09-10 15:51:24
0
khadikskoe1
khadikskoe1 :
allah Akbar
2026-09-10 13:51:29
1
ijumaa.nassoro
IJUMAA 🛸💥🙋🏻‍♂️👥🤝 :
Allah atujalie mwesho mmwem
2026-09-10 17:25:54
0
mimiiy12343
mimiiy1234 :
Tutafsirieni bc kiarabu hatukijuiii🥹kuna watu wana mazambi jamanii
2026-09-10 15:19:15
0
yasinimustafa318
makwazaa :
atar
2026-09-10 12:13:20
0
daa.shuu8
Daa Shuu :
amewasha mwanàdamu kweli lkn je umewaza kwa nn Hy mwanàdamu aka vuke makaburi yt akalifate hilo hp kn nguvu ya Allah pia
2026-09-10 12:24:18
2
To see more videos from user @shebyranco, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About