@sulesh_2025: FUNZO 🥺🤲 Kaburi si mwisho wa maisha, bali ni mwanzo wa safari ya Akhera. Mtume ﷺ ametufundisha kuwa kaburi linaweza kuwa bustani miongoni mwa bustani za Peponi au shimo miongoni mwa mashimo ya Moto. Usisubiri mpaka uingie kaburini ndipo utamani kubadilika. Tubu ukiwa bado una nafasi, swali kwa wakati, acha madhambi na watendee watu wema. Kila mmoja wetu atafika huko siku moja. Ewe Allah, tufanyie makaburi yetu kuwa bustani ya Pepo na utuepushe na adhabu ya kaburi. 🤲😭 #FunzoLaLeo #AdhabuYaKaburi #KumbukumbuYaMauti #IslamicReminder #Sulesh_2025