@insideoutz__: 🔥 MOSE IYOBO ANASEMA MARAFIKI NA USALITI! ❤️🩹 NDIO CHANZO CHA MAHUSIANO YAKE NA AUNTY EZEKIEL KUVUNJIKA💔 Kwenye interview ya moto na Diva The Boss ndani ya (Wasafi FM), dancer nguli Mose Iyobo amevunja ukimya kuhusu penzi lake la zamani na staa wa filamu Aunty Ezekiel. uliozibeba details zote muhimu: 👇🏾🗺️ 📍 Mwanzo wa Safari (Durban, SA): Mioyo yao ilikutana kwa mara ya kwanza nchini Kusini Afrika kwenye Tuzo za MTV Base (MAMAs). Kipindi hicho Wema Sepetu ndio alikuwa mpenzi wa Diamond Platnumz. Ilichukua wiki moja tu ya maongezi na wakawa wameelewana! 🚨 Mpasuko na Chanzo cha Ugomvi: Mose ameweka wazi kuwa "Gang" (marafiki wa karibu wa Aunty) ndio walikuwa chanzo. Walikuwa wanamzushia mambo mengi, na Aunty akawa anaamini maneno ya marafiki zake kuliko ya mwenza wake. 💔 Usaliti na Ukuta wa Mwisho: Mose amedai kuwa usaliti ulizidi kwani Aunty alikuwa ana'mcheat sana. Walijaribu kukaa chini ili kurudiana lakini ilishindikana kabisa, sababu kubwa ikiwa ni Mose alikuwa ameshasogeza maisha yake mbele (moved on). 👉🏾 Marafiki na usaliti viliua penzi lililoanzia Durban. Je, unaamini marafiki wana nguvu ya kuvunja mahusiano ya mastaa? 🗣️👇🏾 #MoseIyobo #AuntyEzekiel #WasafiFM #DivaTheBoss #insideoutz