@millardayo_: Watu watano wamejeruhiwa baada ya lori kupoteza mwelekeo na kugonga vyombo vingine vinne vya usafiri katika Barabara Kuu ya Songea–Njombe, eneo la VETA–Msamala, Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Ruvuma, Melania Nyabwinyo amesema walipofika eneo la ajali walimkuta dereva wa lori amebanwa ndani ya gari hilo ambapo Waokoaji walifanikiwa kumtoa na kumfikisha hospitalini, huku majeruhi wengine wanne wakiwa tayari wamepelekwa hospitalini kwa matibabu. Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Land Cruiser, gari dogo, bajaji na pikipiki ambapo kwa mujibu wa Mashuhuda, Waziri Nchimbi na Thabiti Hamidu, lori hilo lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo kasi huku dereva akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake, kabla ya kukutana na vyombo vya usafiri vilivyokuwa vikitokea upande wa pili. Mashuhuda hao wamesema dereva alijaribu kulirejesha lori upande wake baada ya kushindwa kukamilisha kulipita gari hilo, lakini akashindwa kulidhibiti na kugonga vyombo hivyo. #MillardAyoUPDATES
millardayo
Region: TZ
Friday 11 September 2026 15:23:37 GMT
Music
Download
Comments
SallyM😾 :
mcifanyie challenge hii jamani🥹[Tears of joy][Tears of joy][Tears of joy]
2026-09-11 15:28:05
0
Lora_store :
Madereva wanalewa sana jaman 😭
2026-09-12 18:00:53
1
Jay Meron :
r.i.p mtoto iddi
2026-09-14 11:43:42
0
kauthar nilongo :
wako hai bado au?
2026-09-12 17:51:14
0
neema Michael :
Gen z tunawaomba msiifanyie challenge 🙌🏽🙌🏽
2026-09-11 15:31:50
2
fantana❤️ :
songea yetu jaman
2026-09-12 19:39:00
3
kais wende :
polen
2026-09-14 06:36:27
0
Abrah the Great Tz🇹🇿 :
daaah msela point 15 ndo zimeenda daaaaah
2026-09-11 17:29:37
1
Mwitumba :
tunaishi lakini tunaishia(hayati Brutusi) Amina
2026-09-13 14:31:07
0
johnzacharia188 :
polen sana Wana songea
2026-09-14 16:57:42
0
Ezrah :
jama msifanye chaleenge
2026-09-11 17:26:59
0
Erastus peter :
shida barabara ya songea ni ndogo bwana
2026-09-12 22:32:31
2
FIRST BORN👊🏿5 :
Dah mungu atusaidie barabaran
2026-09-11 15:29:46
0
MR FREEZER :
CHALLENGE ACCEPTED
2026-09-11 15:37:17
0
mpambuki juici 🥑🥰 :
mungu akulaze pahal pema bulutus 😭😭
2026-09-12 18:37:12
0
Eunstore Songea &Dar :
duh🥲🥲
2026-09-11 19:57:16
0
shabia chawandas shabbir :
mbona dereva kishafariki
2026-09-11 21:59:16
0
Dr haluna :
daah
2026-09-11 15:29:13
0
Asha :
poleni,sana
2026-09-15 09:32:48
0
OfficialMo✅🕢 :
poleni
2026-09-11 15:28:32
0
𝐬𝐰𝐚𝐥𝐥𝐨 𝐌𝐂 :
HIII TUNAFANYIA CHALENG [Big LOL][Big LOL][Big LOL][Big LOL][Big LOL]
2026-09-11 15:34:54
1
cratus tz :
garii ndo mbovuu akulewaa bhnaaaaa
2026-09-11 15:48:14
0
Veronicer🍀🩵 :
😭😭😭😭😭
2026-09-11 18:54:54
1
Dr mapunda :
@kazawa
2026-09-11 18:12:07
2
Kidenya :
@Owden De Best 😎
2026-09-11 17:17:22
0
To see more videos from user @millardayo_, please go to the Tikwm
homepage.