@reybellah_10: Kijana Hassan Khamis Rashid (22) ambae ni Dereva wa bodaboda na mkazi wa Beitrasi, amekumbana na Tukio la kuvamiwa na watu waliodaiwa kuwa wezi wa bodaboda katika eneo la Kizimbani, Wilaya ya Magharibi A, Unguja. Kijana Hassan, aliyekuwa akimpeleka abiria kuelekea Kiboje, alivamiwa baada ya abiria huyo kuwasiliana na watu wengine watatu, ambapo alijeruhiwa Vibaya maeneo ya shingoni kwa kitu chenye ncha kali. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi limewakamata watuhumiwa watatu wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo. #reybellah #fypシ #fyp #trending #viralvideo