@kusagatv: “Ni heri mia tano ya mpiga debe anayopata kihalali, standi au kwenye daladala, kuliko mabilioni ya fedha yanayotokana na kumwaga damu. Labda umemuua ndugu yako ili upate fedha, umemuua mama yako au umemuua baba yako.” Haya ni maneno yaliyowahi kusemwa na Mtumishi wa Mungu Abiudi Mishori miaka mingi iliyopita wakati akiimba. Pamoja na kupita kwa muda, ujumbe huu bado unaishi hadi leo na unaendelea kuwa fundisho kuhusu thamani ya maisha, uhalali wa riziki na madhara ya kutafuta utajiri kwa njia ya damu.