@jambotv_: VIDEO: Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, ameipa Serikali pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi muda wa wiki moja kutoa maelezo rasmi kwa umma kuhusu aliko na usalama wa Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Emmanuel Nchimbi, akionya kuwa wakishindwa kufanya hivyo, chama hicho kitachukua hatua za kisheria kuiburuza serikali mahakamani. Ado Shaibu ametoa msimamo huo jana, Septemba 12, 2026, wakati akihitimisha ziara yake katika Mkoa wa kichama wa Kahama baada ya kukutana na wenyeviti na makatibu wa chama hicho ngazi ya mikoa, pamoja na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Kata ya Kagongwa, Jimbo la Kahama Mjini mkoani Shinyanga. Ado Shaibu ameeleza kuwa baada ya kutoa kauli siku chache zilizopita, alitoa fursa ya siku moja kuona kama Dkt. Nchimbi mwenyewe, familia yake, au serikali wangejitokeza kutoa taarifa. Hata hivyo, kutokana na kuendelea kwa ukimya huo, amebainisha kuwa kuna kila dalili za kutilia shaka usalama wake. “Tunataka serikali itueleze Nchimbi yuko wapi, familia yake itueleze Nchimbi yuko wapi au na yeye mwenyewe Nchimbi atoke atuambie yuko wapi…angekuwa salama angejitokeza. Na usalama ninaosema mimi tunataka tujue hali yake ni salama. La pili tunataka tujue anao uhuru wa kutembea…la tatu tunataka kujua ana uhuru wa mawasiliano, atoke tu tumuone. Lasivyo kama hajitokezi tutajua hayuko salama,” amesema Ado Shaibu. Katika hatua nyingine, Ado Shaibu amemshukia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, akimtaka kutambua uzito wa dhamana aliyopewa inayohusu usalama wa raia na mali zao, na inayosimamia vyombo vikuu kama Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto, na Idara ya Uhamiaji.
Jambo TV
Region: TZ
Sunday 13 September 2026 06:24:19 GMT
Music
Download
Comments
princes ney :
hyo imeisha kama pole pole maskin dah inauma san😭😭😭
2026-09-13 14:23:37
0
hernandez hozza :
respect
2026-09-13 12:17:33
1
NGUKU KHAN :
mmmh JAMBO TV😅😂😂😂
2026-09-13 13:59:14
0
yessemlengo :
wamesha muweka lokap mungu amtetee jaman
2026-09-13 12:01:48
7
tik creator 🇹🇯🇹🇯 :
Mungu akulinde zaidi kwa jina la yesu
2026-09-13 13:41:58
5
ccm ya sasa si kama ya zamani, ccm ya sasa ni yakinyama sana
2026-09-13 13:14:46
5
AYATOLLAH ALI KHAMENEI :
nikwer
2026-09-13 06:38:40
3
buruhaniwawa :
tupp pamoja
2026-09-13 14:26:09
1
MR.X :
Kwa maana hiyo Ado ndiyo mwanasiasa peke yake anayeweza kuwa sauti ya Watanzania..Hili swala la Nchimbi linachukuliwa kawaida ila serikali inapaswa kuliangalia vizuri..
2026-09-13 11:53:49
2
ntara j :
tz imebakwa
2026-09-13 14:25:56
1
user3225127199966 :
Mungu amlinde huyu baba jaman
2026-09-13 13:13:09
2
V :
me nko Dunia ya wapi mbona cjh kama kapotea jaman
2026-09-13 13:29:09
1
Khalifa Chuma :
haki haki haki 👑🇹🇿
2026-09-13 10:05:02
2
Lesopla sanlnco :
kweli
2026-09-13 08:42:28
3
dogo sumbu :
tunao tumia wifi tujuanr hapa
2026-09-13 14:11:32
0
user306959797416 :
tena akome
2026-09-13 14:45:27
0
ukhty ishaa! :
asant kunisaidy kuongy baba
2026-09-13 15:38:22
0
user306959797416 :
kweli kabisa spewed rrai
2026-09-13 14:45:55
0
🥰🥰 :
bor umeongea sababu wanataka kmpoteza Kam polepole
2026-09-13 13:55:04
2
pm💞 :
jmn 😭😭😭 Nchimbi
2026-09-13 13:30:08
0
zahasa :
daa ila
2026-09-13 14:04:38
0
Abby Love Clinic :
MUNGU AKULINDE KAMANDA 🙏🙏🙏🙏
2026-09-13 16:06:08
0
👑KING 🦷 :
mimi niko salama nipo na kamshangazi
2026-09-13 14:11:27
0
nay :
Hiiinchi mmmmh
2026-09-13 13:34:41
0
Fungile :
kiongozi mulipata
2026-09-13 08:04:00
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm
homepage.