@jesse_tunuka: Moshi.Moshi. Mwanaume ambaye jina lake halijafahamika amepanda juu ya dari la kanisa na kuanza kujikatakata kwa kisu sehemu mbalimbali za mwili wake , huku akidaiwa kutaka kujitupa kutoka kwenye jengo hilo la ghorofa. Tukio hilo limetokea leo, Jumapili, Septemba 13, 2026, katika Kanisa la River of Joy, Calvary Assemblies of God, linaloongozwa na Mtume Mwamposa, lililopo Mtaa wa Rengua, Kata ya Mawenzi, Moshi Mjini, Mkoa wa Kilimanjaro, wakati ibada ikiendelea. Tukio hilo limesababisha viongozi wa kanisa kutoka ibadani na kuomba msaada wa Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ambao walifika eneo hilo na kufanikiwa kumshusha mwanaume huyo salama. Akizungumza baada ya tukio hilo,Sajenti Meja Martin Mapunda Fluko wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Moshi Mjini amesema walipata taarifa kutoka kwa Inspector Ali majira ya saa 3 asubuhi kuwa kuna mtu anayetaka kujitupa kutoka kwenye jengo hilo la ghorofa. Amesema alipofika eneo la tukio, alimkuta mwanaume huyo amelala juu ya bati, hivyo alizungumza naye kwa lengo la kumshawishi ashuke kwa usalama. “Nilijitambulisha kwake, nikamwambia mimi ni askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, nimekuja na wewe kukupa msaada,” amesema Fluko. Amesema mwanaume huyo alimsikiliza na baadaye akakubali kushuka, ambapo askari hao walimsaidia kufika chini bila kumkamata kwa nguvu. Fluko amesema katika mazungumzo ya awali walibaini kuwa mwanaume huyo alikuwa na matatizo ya kifamilia, huku jina lake likiwa bado halijafahamika. Amesema Jeshi la Zimamoto na Uokoaji litashirikiana na Jeshi la Polisi katika uchunguzi zaidi baada ya mwanaume huyo kutulia. Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, John Swai, aliyefika kanisani hapo asubuhi kwa ajili ya kununua mafuta ya upako, amesema kabla ya mwanaume huyo kupanda juu ya jengo alikutana naye nje ya kanisa na kumweleza kuwa alihitaji kuombewa. #fypシ #viraltiktok

Jesse_Tunuka
Jesse_Tunuka
Open In TikTok:
Region: TZ
Sunday 13 September 2026 13:47:55 GMT
35150
709
52
62

Music

Download

Comments

mushauri.wa.rais
mushauri wa rais :
which country is this?
2026-09-13 16:24:24
0
neema.kdy
neema kdy :
wamwombee jmn
2026-09-13 15:48:56
0
user4925110583800
user4925110583800 :
mmh Sina comment
2026-09-13 15:34:50
0
mrsbee2004
MR'S BEE :
mmmh kama sio irene kashamtenda mtu huko sijui
2026-09-13 15:40:36
7
missjesca3
MRs STEVEN♥️🦋 :
ni Tanzania au
2026-09-13 15:58:28
0
deborahdebby7006
debbycrean :
MUNGU amponye ni mapepo hayo tuendelee kumuombea
2026-09-13 15:57:12
3
trice9d
Trice💎 :
yaan jamani tusali sana
2026-09-13 16:11:52
2
tiwiii557
tiwiii :
happy kwa nn jmonn mpk mwenzio kafikia apoo😂😂😂😂😂😂
2026-09-13 15:52:34
0
elingisongoya3
Elingisongoya :
mungu mponye familia zetu zinatumaliza
2026-09-13 15:39:36
5
consolady1
officiall Conso :
Alokuwa anarekodii mda alitoa wapii jmn🤔
2026-09-13 15:53:12
0
papai.perfume
Tarange -shoes-glama :
Basi wasukuma jamani sisi
2026-09-13 16:04:13
1
user5795821228409
kefle :
ni msukuma
2026-09-13 16:01:21
0
christina.mwasaka
Christina Mwasaka :
Duuuh mungu amponye
2026-09-13 15:13:01
1
azathabass
god is one :
mbn sio kwa bab
2026-09-13 15:39:13
0
user4130036602760
ALICE :
wasukuma mmefikiwa nna ndugu yenu
2026-09-13 16:27:31
0
jackren.official
jackren official :
2026-09-13 16:32:15
0
prisca.kimaro5
Prisca Kimaro :
duuuh🙏
2026-09-13 16:24:17
0
papai.perfume
Tarange -shoes-glama :
Msukuma yamepanda
2026-09-13 16:02:22
1
zanuraabdala810
zanuraabdala810 :
mmmh! si mngemuombea kwanza kabla ya kwenda kituo
2026-09-13 17:48:58
0
agines15
Magreth mmary :
jamni ndio nini sasa hicho
2026-09-13 16:26:38
0
junior.humphrey8
Junior humphrey :
Acheni kuleta taharuki Mwamposa hana kanisa sehemu yeyote zaidi ya kawe dar es salaam, na ndy maana hutamuona sehemu yeyote j,pili zaidi ya kawe
2026-09-13 16:18:06
1
buthalia_hussein
Buthalia_hussein :
Mwamposa na hii moshi kuna kitu unatutafuta
2026-09-13 16:22:18
1
totorimi72
caren1014 :
iren kashamwacha kaka wa watu
2026-09-13 15:58:25
1
rahmamasalu23
rahmamasalu23 :
zimamoto wanazima nini jaman😇🤐
2026-09-13 16:08:01
0
yasini.joseph4
Yasini Joseph :
labda ndo ...............
2026-09-13 15:46:05
0
To see more videos from user @jesse_tunuka, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About