@kaisarashare: Bukan sekadar kopi. Ada bahan untuk fokus dan stamina. Sesuai untuk kerja lama. Try la! #racuntiktok #fyp #kopisehari #stamina #fokus

Kaisara 🌹
Kaisara 🌹
Open In TikTok:
Region: MY
Thursday 17 September 2026 05:10:00 GMT
2
0
0
0

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @kaisarashare, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos

Wazalishaji wa saruji washangazwa bei kupaa mtaani, TRA yakutana nao kujadili Wazalishaji wa Saruji kutoka viwanda vya Twiga Cement na Simba Cement wameonesha kushangazwa na bei kupaa mtaani wakati bei haijaongezeka kwa upande wao. Wazalishaji hao wameeleza hayo leo Septemba 17, 2026, kufuatia ziara iliyofanywa na Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda, katika juhudi za kufuatilia chanzo cha ongezeko la bei na namna TRA inavyoweza kusaidia kupunguza changamoto hiyo.
Wazalishaji wa saruji washangazwa bei kupaa mtaani, TRA yakutana nao kujadili Wazalishaji wa Saruji kutoka viwanda vya Twiga Cement na Simba Cement wameonesha kushangazwa na bei kupaa mtaani wakati bei haijaongezeka kwa upande wao. Wazalishaji hao wameeleza hayo leo Septemba 17, 2026, kufuatia ziara iliyofanywa na Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda, katika juhudi za kufuatilia chanzo cha ongezeko la bei na namna TRA inavyoweza kusaidia kupunguza changamoto hiyo. "Bei tunazoziona kule chini, za kuanzia 21000, 22000 mpaka 23000, zile bei hata sisi wenyewe tunazishangaa, hazipaswi kuwa hivi," ameeleza Meneja Mwandamizi wa Twiga na Simba Cement, Mhandisi Danford Semwenda "Kiwanda kama sisi hatujaweza kuongeza bei tangu tatizo hili lilivyotokea, na pia wale mawakala ambao sisi tunawasimamia hawajaweza kuongeza bei. Uwazi uliopo ni wa pale chini, wale watu warejareja ndiyo ambao wanaweza kuongeza hizo bei," alifafanua Semwenda. Mtaalamu huyo ameleza kuwa uwezo wa uzalishaji saruji nchini ni tani takribani milioni 15, wakati matumizi ni tani milioni 10, jambo ambalo linafanya kama wazalishaji wote wakitumia uwezo wao, suala la upungufu litaondoka. Aidha, alifafanua zaidi kuwa kati ya Juni mpaka Agosti 2026, kwa upande wa Twiga Cement wamezalisha wastani wa tani 160,000 ikiwa ni kiwango cha juu kabisa. Huku kwa kupitia Simba Cement ambapo uzalishaji wa kawaida ni tani 100,000 waliweza kufikia wastani wa kati ya tani 117,000 mpaka tani 120,000. Semwenda ameeleza changamoto kwenye soko ni ya kimsimu ambapo kuanzia mwezi wa saba ambapo mahitaji hupanda baada ya msimu wa mvua kuisha. Hata hivyo ameeleza kuwa katika kikao kilichofanyika kati ya wazalishaji na Wiazara ya Viwanda ilionekana kuwa wazalishaji wawili walikuwa hawajafikia viwango vyao vya uzalishaji. "Uwezo uliopo hapa nchini ni mkubwa kuliko mahitaji, wote tukiweza kuzalisha kama tunavyozalisha hapa Twiga na Simba uhakika ni kwamba hapaswi kuwa na upungufu, na wanaochukua nafasi kuongeza bei kutokana na upungufu haitakuwepo," alieleza zaidi. Kwa upande wa Kamishna wa TRA, Yusuph Mwenda, ameelekeza timu yake ya wataalamu kuendelea kujadiliana na wazalishaji hao kuangalia namna ya kuwawezesha zaidi, lakini pia Mamlaka hiyo imeeleza kuwa itaangalia pia kwa upande wa rejareja ikiwa mabadiliko ya bei yanaonekana katika njia rasmi. "Sasa tutakachofanya, tukiwasikiliza, tutaona ni vitu gani tunaweza kufanya kusaidia gharama zao [za uzalishaji] ziwe chini, lakini pia kucontrol mnyororo mzima wa uuzaji wao," alifafanua Mwenda. Na kuongeza: "Wale wauzaji wa rejareja pia ni walipa kodi, na wao pia tutawafuatilia kama ambavyo tumekuja kwa hawa, ili kuona kile wanachopata ambacho sio cha kawaida — je, kinawekwa wazi? Na kama hakiwi wazi, kwa mujibu wa sheria zetu na taratibu, tutachukua hatua."

About