@salmasaid_znzyetu: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuundwa kwa Kamati ya Pamoja ya Majadiliano yenye wajumbe kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT Wazalendo ni hatua muhimu katika kuendeleza mchakato wa maridhiano na kuimarisha amani, umoja na utulivu wa kisiasa Zanzibar. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 14 Septemba 2026, Ikulu, Zanzibar, alipozindua rasmi Kamati hiyo ya Pamoja ya Majadiliano. Amesema kuundwa kwa Kamati hiyo ni mwendelezo wa utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya CCM na ACT Wazalendo, na kunadhihirisha dhamira ya kuendeleza majadiliano na kuhakikisha hatua zilizokubaliwa zinatekelezwa kwa manufaa ya Zanzibar na wananchi wake. Rais Dkt. Mwinyi amewataka wajumbe wa Kamati kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, kuheshimiana na kufanya kazi kwa ushirikiano, huku wakiweka mbele maslahi mapana ya Zanzibar na mustakabali wa wananchi wake. Amesema wajumbe hao wana jukumu la kuendeleza mazingira ya majadiliano yatakayowezesha makubaliano yaliyofikiwa kutekelezwa kwa vitendo na kuleta matokeo yenye manufaa kwa wananchi. Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa hatua zilizofikiwa katika mchakato wa maridhiano zimejengwa katika misingi ya amani, umoja na mshikamano, ambayo ni muhimu katika kudumisha utulivu wa kisiasa na kijamii pamoja na kuweka mazingira bora ya maendeleo. Amepongeza mchango uliotolewa na viongozi wa CCM, ACT Wazalendo, viongozi wengine wa kisiasa, wazee pamoja na viongozi wastaafu katika kuendeleza maridhiano na kujenga mazingira ya maelewano Zanzibar. Rais Dkt. Mwinyi ametoa shukrani maalum kwa Marais Wastaafu wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume na Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa kuendelea kutoa hekima, ushauri na mchango wao katika hatua mbalimbali za mchakato huo. Amesisitiza umuhimu wa viongozi wa vyama vya siasa na wadau wengine kuendelea kushirikiana katika kuijenga Zanzibar yenye amani, utulivu na maendeleo, akieleza kuwa tofauti za kisiasa hazipaswi kuwa kikwazo katika masuala yanayogusa maslahi ya wananchi na mustakabali wa nchi. Rais Dkt. Mwinyi amesema amani na utulivu vina nafasi kubwa katika maendeleo, kwa kuwa vinawawezesha wananchi kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na shughuli nyingine za maendeleo. Naye, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Mhe. Othman Masoud Othman, amesema chama hicho kiko tayari kuendelea kushirikiana katika kuijenga Zanzibar, huku akimpongeza na kumshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa hatua mbalimbali alizochukua tangu mwanzo wa mchakato wa maridhiano, hususan katika kusimamia majadiliano na utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa. Ameeleza kuwa hatua hizo zimeendelea kuleta matumaini kwa wananchi wa Zanzibar, ambao wana kila sababu ya kutambua na kuthamini juhudi zinazolenga kuimarisha maridhiano, umoja na maendeleo ya nchi. Mapema, Rais Dkt. Mwinyi amekabidhi Hadidu Rejea za Kamati kwa Wenyeviti Wenza wa Kamati, Ndg. Omar Ali Sheikh, Mwenyekiti Mwenza kutoka ACT Wazalendo Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Zanzibar, pamoja na Ndg. Abdi Mahmoud Abdi, Mwenyekiti Mwenza kutoka CCM Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar. Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, viongozi wa vyama vya siasa pamoja na viongozi wa dini.

Salma Said
Salma Said
Open In TikTok:
Region: TZ
Monday 14 September 2026 13:12:43 GMT
12813
597
22
21

Music

Download

Comments

aboudzeko360
dzeko🦅 :
well spoken sir 🙏
2026-09-14 16:07:12
0
bosslee235
boss lee :
mashallah mungu aibariki zanzibar
2026-09-14 18:23:53
2
rampa161
Rampa 🇵🇸 :
Tunaomba iwe kweli tu, Maana hawa wenzetu ni wasanii wakubwa Wallahi
2026-09-14 13:48:22
4
user1009331014732
halima :
omo mungu akutangulie kwa kila hatua
2026-09-14 16:13:00
3
sultan.said28
Sultan Said :
Allah awajaalie kila la kheri biidhnillah
2026-09-14 15:03:13
1
bnmuslim1
bnmuslim :
Inshallah
2026-09-14 15:56:27
2
kemcho.didi
kemcho didi :
ww ndo mweshimi m noma mashaa allha mungu akuline akuweke una naroho ya utu 🥰🥰
2026-09-14 20:03:25
0
salehhilal250
bhaaa :
mh sijui
2026-09-14 20:19:41
0
akaumbo
A Kaumbo :
Hakuna kitu hapo😂
2026-09-14 20:16:00
0
077mk5
Ibrahim :
episode ya ngapi
2026-09-14 18:12:39
1
aysalu6
Aysalu :
inshaallah ameen
2026-09-14 16:05:06
0
mikidadi495
MIKIDADI :
HI
2026-09-14 15:03:31
1
kemcho.didi
kemcho didi :
safii yo
2026-09-14 20:02:12
0
kibona.mpemba
Kibona Mpemba :
Haya subirini matokeo yeye hajui kama kariba uraid
2026-09-14 17:08:53
0
omarhussein5207
omarhussein5207 :
💪💪💪
2026-09-14 15:29:12
0
user24024190945116
user24024190945116 :
🙏🙏🙏🙏✅
2026-09-14 18:04:00
0
To see more videos from user @salmasaid_znzyetu, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About