@jambotv_: VIDEO: Dodoso dhidi ya shahidi wa tano wa upande wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, John Heche, limeendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Dar es Salaam, huku mawakili wa upande wa mashtaka wakijikita katika kuhoji baadhi ya taarifa alizozitoa wakati wa kutoa ushahidi wake. Akijibu maswali ya Wakili Ignas Mwinuka, Heche amesema amewahi kushiriki katika chaguzi kuu tatu za ubunge kupitia CHADEMA, ambapo alishinda katika chaguzi mbili. Heche amekana kwamba katika chaguzi hizo alishuhudia polisi wakijaza kura kwenye masanduku au mawakala wa chama chake kuzuiwa kufanya kazi zao. Pia amesema matokeo ya uchaguzi wa ubunge yanaweza kupingwa katika Mahakama Kuu, lakini amekiri kwamba hakuwahi kupinga matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020. Katika eneo lingine, Heche ameulizwa kuhusu taratibu za wagombea kujaza fomu za kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa. Amesema kujaza fomu ni moja ya vigezo vinavyohitajika, lakini akafafanua kwamba hakujaza mwenyewe fomu ya aliyekuwa mgombea Susan Kiwango, ingawa alisema alihusika katika masuala ya malalamiko yaliyohusiana na uchaguzi huo.
Jambo TV
Region: TZ
Monday 14 September 2026 13:45:27 GMT
Music
Download
Comments
Mtu wa Mungu :
asante kwa kutupasha abali
2026-09-14 16:58:17
3
𝔸𝕣𝕠𝕪𝕔𝕖👊 :
walijua ni mchezo sasa hawamini kinachowatokea
2026-09-14 20:30:29
6
""The Matthew Jr"" :
Mahakama siyo jukwaa la kisiasa ✋
2026-09-14 16:30:21
3
Jimmy :
kesi sio mchezo
2026-09-14 19:51:02
2
Hunter17 :
oya kesi ukihikuta mahakaman, imefika kwa mawakili bs juwa kabisa mawakili hawalali juu yako na iyo kesi ndo ugali wao
2026-09-14 20:34:10
3
አልሀምዱሊላህ አለኩልሀል 💚💛❤️ :
tunawaombea
2026-09-15 05:02:38
0
Nabeel :
Mara hii hakuna Kufunika kombe sheria tu😂😂
2026-09-14 23:10:57
2
Emmanuel🌾jonn🌻🌽🇹🇿🔋 :
😂😂tayari lissu ni mhain
2026-09-14 19:03:39
3
RADIATOR :
Heche amejqmba cheche leo😁👏
2026-09-14 21:02:31
4
Emmanuel🌾jonn🌻🌽🇹🇿🔋 :
mammae kwisha🤣🤣🤣
2026-09-14 19:06:35
4
humble man :
kamendu voice
2026-09-14 19:55:32
0
zaynalbaraaya :
🤣🤣🤣 sasa heche na mawakili nani hajasoma ? wote wamesoma lkn kila MTU anataaluma yake
2026-09-15 06:22:37
0
Miss Nee :
😳😳😳
2026-09-15 00:30:30
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm
homepage.