@bongo_media: Content creator Tibela KT amewakosoa baadhi ya wanawake wanaoingia kwenye mahusiano ya nje ya ndoa, kisha mambo yanapowashinda hurudi kwa waume zao kuomba msamaha huku wakisingizia kuwa “shetani aliwapitia.” Tibela amesema baadhi ya wanawake wanapaswa kujitathmini na kuwajibika kwa maamuzi yao badala ya kutumia visingizio kila wanapokosea. Amehoji: “Unavunja ndoa yako kwa mikono yako mwenyewe, unaingia huko mtaani mambo yanakuwa magumu na yanakushinda, halafu unarudi kwa mume wako kuomba msamaha unadai shetani alinipitia! Hivi huyo shetani alikupitia muende wapi, na baadaye alikuacha wapi?” Amesema badala ya baadhi ya wanawake kusubiri mambo yaharibike nje ya ndoa ndipo wakumbuke umuhimu wa familia zao, wanapaswa kulinda ndoa zao na kurekebisha mapema changamoto zinazojitokeza. Kwa mujibu wa Tibela, mabadiliko ya kweli huanza kwa mtu kujichunguza na kukubali makosa yake, badala ya kutafuta mtu au nguvu nyingine ya kulaumu kila anapofanya uamuzi usio sahihi.