@wepesitv: Bi. Felister Akonaay, mwenye umri wa miaka 60, anatarajiwa kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwezi Novemba mwaka huu katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu, akitoa somo kwamba elimu haina ukomo wa umri. Bi. Felister alihitimu elimu ya msingi mwaka 1982, lakini ndoto yake ya kuendelea na sekondari ilikatizwa na changamoto za kifamilia, ikiwemo kifo cha baba yake. Baada ya kuingia katika maisha ya ndoa, kupata watoto na wajukuu, hakuruhusu changamoto hizo kuifuta ndoto yake. Aliamua kurudi darasani na kuanza masomo ya sekondari, ambapo tayari amemaliza Kidato cha Kwanza na cha Pili na sasa anaendelea kujiandaa kwa mtihani wa Kidato cha Nne. Akieleza sababu ya kurejea shuleni, Bi. Felister amesema alikuwa na ndoto ya kwenda sekondari tangu utotoni, lakini hakupata nafasi kwa wakati huo, hivyo alipoipata fursa baadaye maishani akaamua kuitumia kutimiza ndoto yake. Amewataka vijana kutumia vizuri fursa za elimu walizonazo na kusoma kwa bidii ili kufikia ndoto na malengo yao. Walimu wake wamempongeza kwa juhudi, nidhamu na ujasiri aliouonyesha katika safari yake ya elimu, wakisema amekuwa mfano wa kuigwa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Safari ya Bi. Felister inabeba ujumbe mzito: kuna ndoto zinaweza kuchelewa, lakini kuchelewa hakumaanishi zimekufa.

WEPESI TV
WEPESI TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 15 September 2026 09:41:23 GMT
159756
8134
505
3382

Music

Download

Comments

theddy49
Theddy :
hongerena sanaaaa elimu Haina mwisho
2026-09-15 10:21:55
381
dinasylivester
Dina kagina :
Amenpa nguv Na diploma yangu nisome degree Sasa. 😂😂
2026-09-15 11:52:40
46
pretty45493
shant❤️ :
😳😳😳unatK chet naww😭
2026-09-15 20:08:51
0
itconso
mom Richie😘🥰 :
ningekuwa rafk yake maana atakuwa anajua vitu 😂😂😂
2026-09-15 10:19:49
222
elisha3455
Elimido :
this teaches us to never give up
2026-09-15 18:50:01
1
user1199317940618
Ney julius :
yaan mm Nina miaka 33 nashindwa nn Sasa kusoma??
2026-09-15 10:16:41
92
user3355255177824
sasha :
Nachoka,kama cjaelewa.nina miaka 43 mbn kama nitaweza
2026-09-15 10:12:02
31
angelbless83
Angel bless :
Anasoma akiwa amestaafu tayari ila hongera🥰
2026-09-15 13:06:04
30
the.giant.slayer.07
The Giant slayer🦕 :
umemzid Ex wangu alifeli form two 2021
2026-09-15 11:50:58
2
missjp.19
miss jp :
Basi sina haraka acha nitafute kwanza ada nitarudi
2026-09-15 14:45:25
19
user22949135569408
user22949135569408 :
ndoto lazm zit im is
2026-09-15 11:39:59
2
user99962795496196
N :
au mbingun kuna ajira nrud zangu shule
2026-09-15 10:46:23
12
bonifacepeter0
Badface :
dah me nilikata tamaa kumbe bado safar ndefu aisee. ngoja nikaze
2026-09-15 11:51:48
14
nafsahamis
Nafsa Hamis :
congratulations bibi
2026-09-15 16:35:10
0
lucykidoti01
lucy kidotii :
serikal inakutambua lakin mumy
2026-09-15 10:32:49
11
gagarinho_77
gagarinho_77 :
Ili aje awe naniii?
2026-09-15 11:59:51
6
user86122747262605
Moana 🐚🌊🐬🦀🪷 :
samaani bibi ww ni mchaga au ?
2026-09-15 12:32:45
5
elliana9484
Elliana :
Akimaliza 4m4 tyr kashastaaf sasa itakuwaje ndg serikal 🤔
2026-09-15 12:01:50
10
emanueliniko
mr- niko :
swez soma darasa moja na wazee mie
2026-09-15 10:15:48
12
paskalina995
p :
sasa mm. nan31 yangu nafeli wapi narudi shulee dadekkki daktiiimarto ya gen
2026-09-15 11:07:11
7
kingrobinsontz
King Robinson :
Nipo Dar natafuta mdada tuchangie kodi tuake wote
2026-09-15 18:31:01
1
ky6303
keyyl. :
mi Nina 28 na sithubutu kurudi shule
2026-09-15 15:47:16
3
mishy498
Mishy 😻😻 :
Nipo dar natafuta mkaka tuchangie kod
2026-09-15 19:48:43
3
To see more videos from user @wepesitv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About