@jamiivoice_: HABARI: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amepiga marufuku operesheni za “kamata kamata” za vitega uchumi vinavyotumiwa na vijana kufanya shughuli za kujipatia kipato, ikiwemo baiskeli, bodaboda, bajaji na guta. Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo Septemba 15, 2026 wakati akizungumza na wananchi wa Bariadi mkoani Simiyu, akisisitiza kuwa vijana wanapaswa kupewa nafasi ya kufanya kazi na kujiletea maendeleo. “Nimepiga marufuku kamata kamata ya vitega kazi, iwe baiskeli, bajaji, guta, bodaboda. Wacheni vijana wetu wafanye kazi,” amesema. Ameagiza kuwa baada ya kumalizika kwa ziara yake, endapo kuna baiskeli, pikipiki, bajaji, guta au magari yaliyokamatwa katika operesheni hizo, virejeshwe kwa wahusika ili waendelee na shughuli zao. Waziri Mkuu amesema Serikali inataka wananchi wajikite katika shughuli za uzalishaji na kujiletea maendeleo, huku akisisitiza umuhimu wa maafisa wa Serikali kuheshimu na kuwezesha shughuli za sekta binafsi. Amesema sekta binafsi inatarajiwa kutekeleza sehemu kubwa ya dira ya maendeleo, ikiwemo wafugaji, wakulima, wenye viwanda, mama lishe na waendesha bodaboda, ambao kwa pamoja wanachangia katika uchumi wa nchi. “Lazima kila afisa wa Serikali atengeneze mazingira ya kuwawezesha hawa watu wafanye kazi zao kwa uhuru, amani na kujiletea maendeleo,” amesema. Dkt. Mwigulu pia amewataka watendaji wanaopuuza maelekezo ya Serikali kuacha tabia hiyo, akitoa mfano wa tukio katika mkoa mmoja ambako, licha ya maelekezo yake, alipewa taarifa kuwa mgambo walikuwa wamekamata kifaa cha mama lishe. “Niliwaelekeza mkoa mmoja, kabla sijamaliza ziara nikaambiwa wamekamata kamfuta ya mama lishe. Nikasema hawa hawana adabu, wawekeeni ndani mpaka washika adabu, waone jinsi ilivyo kazi kufanya shughuli za kujiletea maendeleo,” amesema.
Jamii Voice
Region: TZ
Tuesday 15 September 2026 14:41:20 GMT
Music
Download
Comments
#𝗠𝗥 𝗣𝗢𝗦𝗛𝗢 𝗚𝗣 :
Asante 🫡
2026-09-16 11:57:07
0
Yunu Boy :
Wanayoongea viongozi na yanayotendeka huku mjini ni vitu viwili tofauti.mfano Hapa Dar maguta.pikipiki.bajaj.mama lishe wanateswa mno.Mheshimiwa waziri mkuu
2026-09-16 09:23:12
4
Isaack :
baba ukiwraixi.mimina,kup,kura,hadi mtoto.wangu,aliye2mboni.nayeeankupakura,hatakwfimbo
2026-09-16 11:30:38
1
apollo Issa :
vitendo vitendeke mkuu wetu asnte san
2026-09-16 08:18:46
1
ye :
safi kaka
2026-09-16 11:56:55
0
Husna :
mm wamenibebea adi besen lamiogo kaliakoo
2026-09-16 11:52:30
0
shai :
asie kupenda kapenda iyooooo
2026-09-16 10:52:05
0
user5489999807401 :
Asante waziri mkuu hiyo iwe sheria
2026-09-16 07:12:20
1
Ramadhan ngoz :
tatiz bado wanakamat wanapinga kauli yak baba
2026-09-16 08:19:36
1
Frank de jong jr :
mbona dar huk nitofauti yani tunawindana tu
2026-09-16 12:05:59
0
vester :
ii yalini
2026-09-16 11:05:40
0
stephano samwer❤️❤️❤️❤️ :
asate.kaka.ubalikiwe.naomba.kuogeya.naww.
2026-09-16 11:35:32
0
Juma Ndaro :
Naomba uje na huku dar uwape darasa
2026-09-16 11:13:35
0
@benjamin.mzee :
mungu akubaliki sana mkuu
2026-09-16 10:42:04
0
OUSMAN 551 :
baba njoo huku dar tunanyanyasika mpka tunalia kusema ukweli
2026-09-16 11:50:39
0
fataelymarcko :
makufuli WA pili uyu kiongozi anae jua aza zetu. mungu mlinde
2026-09-16 11:13:32
0
NOVER TZ...🇹🇿 :
namuombea sana awe raisi mzee kazi inamfaa
2026-09-16 11:19:48
0
julius saitoti :
umeongea ukweli police wametumaliza kwali
2026-09-16 07:01:54
0
JEY D :
vitendo vitendeke mkuu kasema
2026-09-16 10:37:48
0
♥️♥️familia 🫶🫶♥️♥️♥️ :
Mh mbona Bado wanatukamatatu kaliako Hawa Jiji iyo imekaaje mheshimiwa
2026-09-16 10:33:45
0
Stanley Ndile :
dah kama itatekelezwa ni nzuli
2026-09-16 12:11:26
0
queeanna :
bora maana wez wangekuwa wengi sana h0ngera sana
2026-09-16 10:37:53
0
Abeid Seif :
hongera waziri mkuu
2026-09-16 10:35:50
0
Bangoloo :
Hongera sana waziri mkuu
2026-09-16 10:33:46
0
Stella :
kariakoo nililia baba anauza machugwa migambo wakachukua😭😭
2026-09-16 07:12:58
0
To see more videos from user @jamiivoice_, please go to the Tikwm
homepage.