@wepesitv: Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka vijana wa Kitanzania wachangamkie fursa zilizopo katika sekta ya madini ili wanufaike na utajiri wa rasilimali hizo na kujenga biashara kubwa za Kitanzania. Amesema Serikali inalenga kuwawezesha wachimbaji wadogo kukua na kuwa wawekezaji wakubwa, akisisitiza kuwa rasilimali za madini zinapaswa kuwanufaisha Watanzania. "Tunataka wachimbaji hawa wadogo nao wakue, tutengeneze mabilionea wa Kitanzania; ndiyo maana rasilimali hizi zililetwa hapa Tanzania ziwanufaishe Watanzania," amesema. Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Septemba 15, 2026) wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Sapiwi, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, katika ziara yake ya kikazi mkoani humo. Waziri Mkuu amesema baadhi ya watu wamekuwa wakishikilia idadi kubwa ya leseni za madini kwa miaka mingi bila kuziendeleza, huku vijana wakikosa maeneo ya kufanya shughuli za uchimbaji. "Mtu mmoja anakuwa na leseni nyingi, ameshikilia miaka 10, vijana wanatafuta pa kuchimba... hili nimemwelekeza Waziri wa Madini afanye tathmini, aliye na leseni asiyoifanyia kazi, apewe vijana wapate pa kuchimba," amesema.

WEPESI TV
WEPESI TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 15 September 2026 15:13:27 GMT
4589
113
6
12

Music

Download

Comments

thomsg0748480456
ThomasSG :
jaman
2026-09-15 22:26:41
0
nghumbo.malugu.ki
king 👑👑 lyamgoko :
utachukuaje hatua mkuu ambapo ukienda wizarani wanahitaji kuweka watu hao ambao wanawaandaa wao kama waooo@mwigulu nchemba
2026-09-15 22:12:21
0
user6158021921767
user6158021921767 :
🥰🥰🥰🥰🥰🥰👍👍👍👍👍👍👍👍👍asante mwiguruuuu mungu akutunze namama samiaaa
2026-09-15 16:19:08
0
user4047952502046
jiko la oil chafu :
sawa mzee
2026-09-15 16:45:53
0
ramadhaniabdala4
ramadhaniabdala4 :
Hapo sawa
2026-09-15 21:19:36
0
To see more videos from user @wepesitv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About