@kanikibrown: TUWE MAKINI, TUSUBIRI UKWELI. -ALPHONCE MUYINGA-TUWE MAKINI, TUSUBIRI UKWELI Mzee wa TEC anasema yeye kama Mzee wa TEC na taasisi za kidini hawaruhusiwi kwenda kwenye vituo vya kupigia kura kujua nani alipiga kura na nani hakupiga kura. Anasema matokeo waliyonayo ni yale waliyopewa na mamlaka husika. Lakini baadaye anasema tena kwamba siku ya uchaguzi watu hawakwenda kupiga kura kabisa, vituo vilikuwa wazi, hata huko vijijini watu hawakupiga kura. Sasa kwa kauli zake mwenyewe, anasema ni vigumu kujua ukweli ni upi. Anauliza pia, hizo asilimia 30 zilitoka wapi? Anakazia suala la watu waliouawa, lakini hasemi nani alichochea vurugu hizo. Hasemi lengo la vurugu lilikuwa nini. Je, zilikuwa vurugu za kawaida au kulikuwa na mpango wa kuvuruga uchaguzi na kukinukisha? (MAPINDUZI) Hasemi nani alidhamini au kuzifadhili harakati hizo, wala nani alizidhaminiwa. Hasemi pia kuhusu watu waliokatwa vidole kwa sababu ya kwenda kupiga kura. Hasemi kuhusu watu waliochomewa magari na mali zao kwa sababu walikwenda kupiga kura. Wala hasemi kuhusu chuki za kisiasa zilizopandikizwa ambazo zilifikia hatua ya mali zilizodhaniwa kuwa za viongozi au wanachama wa chama fulani kuteketezwa. Watanzania tuwe makini. Tusihukumu kwa hisia wala kwa taarifa za upande mmoja. Tusubiri Tume ya Mheshimiwa Rais itueleze kwa ushahidi: nani alifadhili, nani alifadhiliwa, nani alichochea, nani alihusika, na kwa namna gani alihusika. Ukweli ni muhimu kuliko propaganda. Tanzania inahitaji ukweli, haki, amani na uwajibikaji. 🔴Ukiwa na HABARI MPIGIE RIPOTA 0622732287 RIPOTA WA HABARI ZA MIKOANI ✍ @kaniki_brown #Ripotawahabarizamikoani #kanikibrown #WeweNiFamilia
Kaniki Brown
Region: TZ
Tuesday 15 September 2026 16:24:50 GMT
Music
Download
Comments
imma :
mwambie
2026-09-15 18:37:02
0
ZeffaT :
DUUUUUUUU!!!!
2026-09-15 18:17:39
0
Emma Malenga :
hata mimi nilienda kupiga kura na tulikuwa wengi tu
2026-09-15 19:46:16
1
Jimmy :
Facts
2026-09-15 19:52:19
1
Hamis Ramadhan :
nikweli kabisa
2026-09-15 18:20:09
1
Nyabange :
achana na hayo kwanza nani aliwaua watu
hili ndio kubwa kuliko yote
2026-09-15 19:24:57
0
user8011754507566 :
kumbe napolice walikufa
2026-09-15 20:40:36
0
Ochu :
Mzee wa tec anaajenda yake ya siri
2026-09-15 17:34:58
1
Specialist 🚚 :
Ni Kweli hatukwenda mm nilitaka kutoka kwenda kupiga kura nikarudishwa na marisasi 😥😥😥😥😥😥😥😥
2026-09-15 21:40:33
0
lone jr :
😂😂😂😂 asee kun mambo hi tanzania
2026-09-15 20:02:34
0
Hanifa Urassa :
Tulipiga kura watu wengi sana, Kitima anahangaka nini
2026-09-15 20:20:21
0
EDD😎 :
Blan wash ni nn?
2026-09-15 19:54:00
0
gtwice1 :
unachambua kwa nguvu nyingi jambo dogo sana ... tumia hio nguvu uchambua haki Mzee hata wewe unafanya hayo ukitegemea upewe haki yako
2026-09-15 22:31:24
0
Rajabu Makuka :
nikweli kaka uyumzee achunguzwe
2026-09-15 21:00:12
0
Denis kinunda :
ipo siku wewe jamaa.naludia iposiku nasema Tena iposiku.niswala la muda tukijana
2026-09-15 20:09:35
0
Gian :
kweli lkn rekebisha lugha kwanza sio kula ni Kura sio location ni location na sio asemi ni hasemi
2026-09-15 18:40:35
0
Jimmy :
bahati nzuri tuna wakili msomi Katuga
2026-09-15 19:54:33
0
Jimmy :
usiwe na wasiwasi Kaka, huyo Mzee wa Tec anasubiriwa na wakili msomi Katuga
2026-09-15 19:53:37
0
halidymafitaa :
wanashidwa kuwa wakweli tuitwe nasisi tuseme ukweli mm siyo ccm la nani ..l
kwann wakwepwa kusema ukweli ..
2026-09-15 17:20:20
0
Michael Martine :
hata hufanan
2026-09-15 16:40:34
0
Ahmed Iddy :
hakuna tumeeeee bwanaaa
2026-09-15 18:09:55
0
piusi mangumi :
wtz tunajua ukweri siyo wajinga
2026-09-15 19:47:42
1
HamoodVibe :
Hawezi kusema
2026-09-15 17:31:33
0
hebronmwamwaja :
njaaa mbaya sana
2026-09-15 18:31:05
1
user5819104873346 :
njaa imekuwa kali papa Tv
2026-09-15 16:54:57
0
To see more videos from user @kanikibrown, please go to the Tikwm
homepage.