@jambotv_: VIDEO: Dodoso dhidi ya shahidi wa tano wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, John Heche, limefikia mwisho baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Nassor Katuga kumaliza kumuuliza maswali. Katika sehemu ya mwisho ya dodoso, Wakili Katuga alimtaka Heche kuwaeleza majaji kwamba mtu anapotishia kuvunja amani, anakuwa anamtisha nani, ambapo Heche alijibu kuwa hajui. Wakili Katuga alirejea kauli ya Heche kuhusu hotuba ya Jaji Chande kwamba haikuwa na majina ya waliouawa na waliowaua, akitaka kujua kama alikuwa akizungumzia Katiba au taarifa. Heche alisema ni taarifa, na alipoulizwa kama aliisoma au kuisikia, akasema aliisoma. Alipoulizwa kama ni taarifa au ripoti, Heche alisema hajui. Wakili Katuga pia alimuuliza Heche kama anafahamu kuwa taarifa ya Jaji Chande ilikabidhiwa kwa Rais, ambapo Heche alisema anajua kwa sababu walisema kwamba wamemkabidhi. Katika hoja nyingine, Wakili Katuga alirejea kauli ya Heche kwamba katika hotuba ya Jaji Chande hakukuwa na majina ya waliouawa na waliowaua, magari yaliyochomwa moto na mengineyo, na kumuuliza kama huo ni ushahidi aliousoma au kuusikia. Heche alisema unatokana na hotuba na mambo aliyosikia.

Jambo TV
Jambo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 15 September 2026 18:02:23 GMT
48014
1255
29
68

Music

Download

Comments

fimbo773
""The Matthew Jr"" :
Mahakama siyo jukwaa la kisiasa ✋
2026-09-15 19:48:34
7
jojooh68
jojooh :
Hasa hayo ya yaingiaje hapo na kesi ya uhaini
2026-09-16 12:09:15
2
neemawamboo
ndemwa :
watanzania hawajui sheria za nchi yao.dio maana serikali ya tz ilikataa ma lawyer wa kutoka kenya.kuigia kuitetea upizani
2026-09-15 22:08:40
2
user8171505539933
user8171505539933 :
heche sijui
2026-09-16 09:10:51
1
yahya.majid48
Yahya Majid :
sijui siju 😅😅😅
2026-09-17 04:59:22
1
aishahabs01
Aisha Habs :
dah safii san
2026-09-17 12:07:24
0
jovincom
jovin com :
mh niko pamoja nanyi
2026-09-16 05:33:18
0
victoria.gl20
Victoria GL :
we acha tu Sasa hivi nikisikia Kuna dodoso wallah natimua mbio, dodoso sio poa kabisa
2026-09-15 19:50:28
6
samah_serum
samah_serum :
lissu ahukumiwe hafai kukaa uraiani alichochea vurugu ikagharimu maisha ya watanzania heche ni tapeli ni mwizi
2026-09-15 18:37:00
14
zfdctv
ZFDC TV :
huyu Heche ajielewi
2026-09-16 04:43:47
2
user698339674177
user698339674177 :
hajui hajui hajui
2026-09-16 10:30:28
1
mobaaroos
OfficialMo✅🕢 :
Ila Mbweecheee [Tears of joy][Big LOL][Tears of joy]
2026-09-15 21:38:56
1
exavery1234
daniel :
SEMA HECHE KWENYE MASWALA YA SHELIA YUKO DOW KABISA😳😳😳
2026-09-18 04:35:01
0
elisha81555
ELISHA 🇹🇿. 🇲🇿 ❣️❣️ :
🥰🥰🥰
2026-09-16 12:01:34
1
user4429976308174
Hamad12887 :
😳😳😳
2026-09-16 03:31:03
0
ibrahimsuleiman194
Ibrahim Suleiman :
[Big LOL]
2026-09-16 04:17:04
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About