@smpmedia1: Wakati mwingine unaweza usijue hata wewe mwenyewe chanzo cha changamoto unazopitia. Mwanaume huyu alichorwa picha ya kifaranga kichwani bila yeye kujua. Kila alipokwenda, kunguru alimfuata kwa sababu aliamini kwamba yule alikuwa kifaranga halisi. Hata aliyempakia kwenye bodaboda hakujua kinachoendelea, mpaka usumbufu wa kunguru ukasababisha ajali. Funzo la maisha ni hili: Kuna wakati unapitia changamoto moja baada ya nyingine, unajiuliza, “Kwa nini mambo haya yanatokea kwangu?” Kumbe kuna jambo nyuma yako ambalo hulijui, au kuna mtu anayefanya jambo linaloweza kukuweka kwenye hatari bila wewe kufahamu. Wakati mwingine watu wanaweza kufanya mambo yanayokuathiri, kukuweka kwenye mazingira magumu au kukusababishia madhara, huku wewe ukiendelea na maisha bila kujua chanzo. Ndiyo maana si kila changamoto unayokutana nayo inaonekana chanzo chake mara moja. Kuwa makini na watu wanaokuzunguka. Kuwa makini na mambo unayoruhusu kwenye maisha yako. Na usipuuze ishara ndogo zinapojirudia. “Si kila vita unayopigana unaijua ilianzia wapi.” Smart Musabalala Wakati mwingine unahitaji kusimama, kutafakari na kujiuliza: “Ni nini kinachosababisha haya yote?” Kwa sababu huenda tatizo unaloliona mbele yako ni matokeo tu na chanzo chake kiko sehemu ambayo hujawahi kuiangalia. by Smart musabalalaa @smpmedia1 #LifeLessons #Wisdom #Mindset #SelfAwareness #Maisha
SMP MEDIA
Region: TZ
Wednesday 16 September 2026 07:48:53 GMT
Music
Download
Comments
There are no more comments for this video.
To see more videos from user @smpmedia1, please go to the Tikwm
homepage.