@uhondo.tv: Madereva wa daladala katika eneo la Kizota Mnada Mpya jijini Dodoma wamesitisha shughuli zao, wakilalamikia hali ya miundombinu ya stendi hiyo na mazingira wanayosema hayawawezeshi kufanya shughuli zao kwa ufanisi. Madereva hao wamesema wamekuwa wakielekezwa kuingia ndani ya stendi kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria, lakini wanadai eneo hilo halina baadhi ya huduma muhimu, ikiwemo vyoo na umeme, huku wakieleza kuwa baadhi ya maeneo yana changamoto ya maji. Kwa mujibu wa madereva hao, hali hiyo imewafanya baadhi yao kuendelea kupaki magari nje ya stendi, kando ya barabara, wakitafuta maeneo ya kupata abiria. Mmoja wa madereva hao amesema hawana nia ya kupingana na Serikali, bali wanaiomba Serikali kuangalia changamoto hizo na kuhakikisha stendi inakamilishwa na kuwekwa katika mazingira yanayowawezesha kufanya shughuli zao kwa utaratibu. “Sisi tunaiheshimu Serikali, sisi ni watiifu. Tunaiomba Serikali itusaidie, kwa sababu kule ndani hakuna choo, hakuna umeme na kuna changamoto za miundombinu,” amesema dereva huyo. Madereva hao pia wameeleza kuwa wanahitaji maeneo ya kupakia na kushusha abiria yapangwe vizuri, wakisema kukamilika kwa stendi kutasaidia kuondoa changamoto wanazokutana nazo kwa sasa. Mgomo huo umeibua hali ya kutokuwepo kwa huduma za kawaida za usafiri katika eneo hilo, huku madereva wakisisitiza kuwa wanachohitaji ni utatuzi wa changamoto za stendi ili waweze kuendelea na shughuli zao kwa usalama na utaratibu. #UhondoTVUPDATES
Uhondo TV
Region: TZ
Wednesday 16 September 2026 12:44:06 GMT
Music
Download
Comments
Miss Kiwia :
sawa leo mmetunyoosha 🙌🙌🙌🧎
2026-09-16 13:38:23
10
MkomochiSosbzo :
Kwa Ufupi Mkoa Wangu Jiji langu la Dodoma Bado halina miundombinu ya stend za Daladala. kidogo stand ambayo ilikuwaga na hadh kigogo ile iliyohamishwa ya jamatini.
2026-09-16 13:32:20
19
Bushiri Seifu :
yatapitatu
2026-09-16 18:16:34
3
danilist :
nakubal wanang
2026-09-17 01:29:08
1
AMKA na BBC :
hiyo nimeipenda nasisi wamaloli tunaelekea kugoma kazi
2026-09-16 14:41:29
3
habibalucy :
mmhh sijui tunaenda wap mambo vuruvuru
2026-09-16 17:41:04
2
swai :
kilaa mahali CCM hoye
2026-09-16 20:40:59
2
najma 123 :
jamani tumeteseka sana leo
2026-09-16 18:40:10
3
Emanueli Kisetu :
Hata huku stendi yamkoa 88 miaka yote mabasi yalikua hayapo maana kila mwenye basi alikua nakituo chake sasa selikali imepambana imeyarudisha mabasi tuna siku 5tu migambo wajiji takukuru tbc asa mbina hayo yote hayakuwepo au ndio penye riziki hapakosi fitina!?
2026-09-17 10:15:48
0
loningo16 :
hii mpak ieleweke
2026-09-16 18:52:16
1
dalfa,c :
wamekata kwangu jmn hata msiulize waya .ni ofsni kwangu jmn
2026-09-16 18:26:34
1
its.Eunice❤🌹 :
kwaniniii
2026-09-16 16:31:53
0
MkomochiSosbzo :
Soko la Machinga limejengwa vizuri wakasahau Space yakuweka stand.
2026-09-17 07:12:26
0
I.t.s.NAJIE🦋 :
Mtagini Mavunde
2026-09-16 15:50:51
3
Ado778 ✨💤💥💥 :
vibajaji vinateka apo mtaacha ndala 2 maana
2026-09-16 19:24:08
1
Ester Njukula :
ndo maana nilipita nikakuta kumepoa [Snicker][Snicker][Snicker][Snicker][Snicker]
2026-09-16 15:17:11
2
mwajay cut :
kwani samia bado yupo msibani
2026-09-17 08:42:41
0
fabyrider :
😳😳😳
2026-09-16 20:23:41
1
kibomaster7 :
👏👏👏
2026-09-16 20:15:15
1
SENA BOY :
🥰🥰🥰
2026-09-16 17:25:09
1
EDIGA YOU🧎♂️ :
🥰🥰🥰
2026-09-16 12:54:07
2
To see more videos from user @uhondo.tv, please go to the Tikwm
homepage.