@jambotv_: VIDEO: Katika kuendelea kwa maswali ya ufafanuzi ya Lissu kwa shahidi wake wa tano, John Heche, leo Septemba 16, 2026, Lissu amemtaka Heche afafanue majibu yake kuhusu ripoti za waangalizi na taasisi za kimataifa kama SADC na kueleza kile kilichosemwa mbele ya majaji kuhusu suala la utekaji. Heche amefafanua kwamba katika ukurasa wa 6 wa ripoti hiyo ya SADC, ulizungumzia masuala ya utekaji. Kutokana na Jibu hilo, Wakili wa Serikali Mkuu Nassor Katuga, alisimama na kupinga na kueleza kuwa hicho ni kipengele cha Re examination na siyo Examination in Chief, akidai kuwa Heche anaanza kusema mambo mapya. Tundu Lissu alijibu madai hayo ya Wakili wa Serikali Mkuu Nassor Katuga kuwa, kitu anachokubaliana na Wakili huyo ni kutajwa kwa ukurasa wa 6 pekee ambao awali shahidi hakuutaja, akisema mengine yote yaliyosemwa na shahidi yalikuwa sahihi. Lissu aliendelea kumuuliza Heche amwonyeshe kwenye ripoti ya SADC kuhusu utekaji pale aliposoma ili afafanue, na Heche alithibitisha kuwa ni kweli kwenye ripoti hiyo ya SADC ilizungumzia pia suala la utekaji.

Jambo TV
Jambo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 16 September 2026 15:25:19 GMT
16575
432
5
14

Music

Download

Comments

merry.riziki
Merry Riziki :
hamna shida si watarudi tuu !!!
2026-09-17 12:13:08
0
victoria.gl20
Victoria GL :
wameenda masomoni watarudi 2032
2026-09-16 17:28:00
0
douglasalpho
douglasalpho :
waongo leo nimeuona msafara wa IGP akirud hom jion hii
2026-09-16 18:28:43
1
sameerfashion06
SAMEER FASHION :
[Heartwarming]
2026-09-16 18:30:44
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About