@focustvtz: Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limefanya operesheni maalum usiku na kuwakamata madereva kadhaa wa magari yanayokwenda nje ya nchi (IT) katika eneo la ukaguzi la Ruaha Mbuyuni, mkoani Iringa, kwa makosa ya kuendesha kwa mwendo kasi na kuyapita magari mengine (overtaking) bila kuangalia usalama. Operesheni hiyo ya pamoja imewakutanisha Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, (SSP) Gabriel Chiguma, na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, (SP) Glory Mtui, ikiwa ni mkakati wa kukabili ukiukwaji wa sheria za barabarani kwenye Mstari wa TanZam. Kilichotokea ni kwamba, wakati madereva hao wanakimbizana Barabarani kutokea Morogoro kwenda Iringa, hawakujua kama RTO wa Morogoro naye anaelekea Iringa. Katika operesheni hiyo, makumi ya madereva walipigwa faini za papo kwa papo, huku wengine wakipewa elimu ya usalama barabarani na maonyo makali kuhusu ushupavu wa kuvunja sheria. #FocusTVTanzania
Focus TV Tanzania
Region: TZ
Thursday 17 September 2026 04:25:02 GMT
Music
Download
Comments
mawio🌄🌇 :
Mazda CX-5 💀
2026-09-17 10:52:38
1
Chris frank :
askari kama hawa ndo tunao wahitaji anaongea na raia friendly na piah anakuwajibisha hii ndo Tanzania tunayoitaka
2026-09-17 06:07:19
22
Willy Mjukuu :
Sema askari anaongea kishkaji sana tena kwa point muhim sana Mungu akulinde bro....
2026-09-17 05:42:40
43
kidda2000 🇹🇿 :
respect
2026-09-17 06:57:53
0
baba tony :
uyooo kamanda anakuaga poa sana
2026-09-17 06:47:35
6
inco kenzie :
tanzania ni ngumu, huku kenya polisi ni either uhepe, hawatakifutwa, ukisimama uwapee chai ama upewe ticket, story mingi na vitisho hakuna
2026-09-17 05:32:44
4
Apollo :
askari kama huyo hata akikuandikia fine hata huumii coz anakupa maelekezo kwanza kabla ya yote
2026-09-17 06:27:01
7
MAGARI USED TANZANIA :
aisee iyo Mazda kuipata rabda dereva awe ajui garii kile kisanga kingine kwenye mbioo
2026-09-17 06:22:26
4
hansy daddyz🏍🧢 :
jamaa anaongea kwa point sana
2026-09-17 06:06:33
4
Magulu Nnyondo :
kweli mkuu usalama ni wakila mmoja tuzingatie usalama wa barabarani
2026-09-17 09:58:50
1
Seth Ndagiwe :
afande RTO safi sana mungu akulinde akupe maisha marefu kwa maelekezo kwa vijana
2026-09-17 06:59:47
2
Jr :
RTO Mororgoro apewe Maua yake... Hiii ndo namna ya kuongea na Madereva.. Lazima tuwe Friendly ili tuelewane
2026-09-17 07:48:03
2
Mercedes-Benz Ujerumani :
Asante afande ubarikiwe sana yaani ukimwelekeza dereva hivyo anaelewa sana kuliko kumshurutisha
2026-09-17 10:06:04
1
denisgabi17 :
Salute kwako Mkuu
2026-09-17 05:30:06
3
ALL ABOUT BUSES BACK UP🇹🇿 :
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍 𝐖𝐀𝐒𝐈𝐎𝐕𝐀𝐓𝐄𝐊
2026-09-17 05:21:10
0
TATA BM🦅🇹🇿(Newman) :
BADO KUNA ASKARI WEMA SIO KAMA SIKU ILE WALIKUWA WOTE
2026-09-17 12:59:00
0
Luhkel Luh :
katuchelewesha. bn.
2026-09-17 11:06:49
0
kwahao jamaa siwezi kuwa tetea
2026-09-17 05:09:30
0
calvincalvin2719 :
Sehemu zote za Umma kungekuwa na watu Kama huyo Afande Ingekuwa unyama sana… ingefika muda mtu kufanya upuuzi anaona haya mwenyewe.. Mungu ambariki..🙏
2026-09-17 06:04:23
0
Khalfan Jembe :
🫡🫡🫡🫡
2026-09-17 06:51:29
0
dannylolo :
2026-09-17 07:40:24
0
Sylivesta Enock :
pamoja sana afende
2026-09-17 13:09:34
0
Tandah store :
Kwahiyo point zimepungua au ?
2026-09-17 07:04:36
0
Lusogo Albert :
hiii nikweli kabisa yaani daaah 🙌🙌👍
2026-09-17 08:09:47
0
CBB837T :
wangetanua barabara hiyo ayse tukisema Tufwate sheria tunduma tutatumia siku 3 wewe saiv folen hiyo ya barabara ya Tazama haielezek ni kutoka dar mpaka tunduma n folen Sasa kwann usiover take kwanza mimi naona waongeze ufanisi na barabara speed 50 ni ndogo sana magar n mengi kuzid barabara
2026-09-17 08:31:10
0
To see more videos from user @focustvtz, please go to the Tikwm
homepage.