@health_farm_tz: DR. LUKA MKENI anaeleza kuhusu uwepo wa kemikali zinazoweza kuzalishwa wakati wa upikaji na usindikaji wa nyama, ambazo zimehusishwa na ongezeko la hatari ya saratani, ikiwemo saratani ya utumbo mpana. Upikaji wa nyama kwa joto kali, hasa kuchoma, kuoka au kukaanga, unaweza kuzalisha kemikali kama Polycyclic Aromatic Hydrocarbons (PAHs) na Heterocyclic Amines (HCAs). Aidha, nyama zilizosindikwa kama sausage zinaweza kuwa na misombo ya N-nitroso, ikiwemo nitrosamines, ambayo imehusishwa na hatari ya saratani. Hivyo, aina ya nyama, kiasi kinacholiwa na namna inavyopikwa au kusindikwa ni mambo muhimu ya kuzingatia katika ulaji wa nyama. Aidha, Kumbuka kuwa kwa mujibu wa GLOBOCAN 2022, Saratani ya Utumbo mpana ni saratani inayoshika nafasi ya 5 katika orodha ya saratani zinazoongoza nchini Tanzania huku saratani ya Shingo ya kizazi ikiongoza kwa wanawake na saratani ya tezi dume ikiongoza kwa wanaume. ELIMIKA, HAMASIKA, CHUKUA HATUA KABLA MWILI HAUJACHOKA! CREDIT: wasafiMedia & Dr Luca Mkeni #healthfarmtz #nyama #saratani #tiktoktanzania #afya

health_farm_tz
health_farm_tz
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 17 September 2026 05:24:17 GMT
6401
79
6
91

Music

Download

Comments

sally5......5
Salma :
wagonjwa watarajiwa wako weng Mwenyezi Mungu tusaidie
2026-09-17 15:44:46
2
aryborn
user4921157175675 :
tuleni tu , bila nyama mambo yatakuwaje
2026-09-17 16:21:19
2
rama.kazili
Rama Kazili :
Tulenini sana
2026-09-18 06:47:45
0
user2252817835177
Omega :
duh
2026-09-17 19:32:06
0
ruger133
Abuu Abdillah Assalafiyya :
🙏
2026-09-17 05:46:06
1
majani.mabichi2
Majani Mabichi :
nisikilizeni mimi kuleni Nyama. Mboga mboga zina Madawa
2026-09-18 06:16:39
0
To see more videos from user @health_farm_tz, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About