@chawamata_tv: VIDEO: Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, SACP William Mkonda, amesema kabla ya kuanza utekelezaji wa Mfumo wa Pointi kwenye leseni za udereva, Jeshi la Polisi linatarajia kutoa elimu ya kutosha kwa madereva na wadau wa usalama barabarani. SACP Mkonda amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kubaini kuwepo kwa mashaka na taarifa zinazozagaa katika makundi ya WhatsApp na maeneo mengine kuhusu mfumo huo, akisisitiza kuwa kanuni ipo tayari, lakini elimu inapaswa kutolewa kwanza kabla ya utekelezaji wake. Amesema katika zoezi hilo watatoa vipeperushi vyenye maelezo kuhusu namna mfumo huo utakavyofanya kazi, makosa yanayoweza kuhusishwa na pointi pamoja na mambo ambayo madereva wanapaswa kuyafahamu ili kujilinda dhidi ya ukiukaji wa sheria. Aidha, SACP Mkonda amekanusha taarifa kwamba kwa sasa madereva wanapopewa tiketi za makosa ya barabarani wanakatwa pointi kwenye leseni zao, akieleza kuwa alama zinazoonekana kwenye mfumo zilikuwepo tangu kipindi cha majaribio cha mwaka 2014 na hazimaanishi kuwa pointi mpya zimekatwa kwenye leseni za madereva. Amesema ili pointi ziweze kuhusishwa moja kwa moja na leseni ya dereva, mfumo huo unatakiwa kuunganishwa na mfumo wa mamlaka inayohusika na utoaji wa leseni. SACP Mkonda amewataka viongozi wa madereva na wadau wengine kuwa sehemu ya kutoa elimu badala ya kueneza taarifa zisizo sahihi, akisisitiza kuwa viongozi wanapaswa kuwa walimu na kusema ukweli kwa wanachama wao. Amesema lengo ni kuhakikisha elimu ya kutosha inatolewa na changamoto zilizobainishwa na viongozi wa madereva zinashughulikiwa kabla ya kuanza utekelezaji kamili wa mfumo huo. #ChawamataTV #10KFollowers #Asanteni #ChawamataTV #10KFollowers #Asanteni #ChawamataTV #10KFollowers #Asanteni #DarEsSalaam #Tanzania #Bongo #Habari #HabariLeo #BreakingNewsTZ #TanzaniaNews #BongoUpdates #TzUpdates #TzNews #BongoMedia #MediaTanzania #OnlineTV #trendingréels #tanzaniatrending #polisiviral #Asanteni #tanzaniatrending_habari #tanzaniatrendingsong #mediatanzania #tanzaniatrendingvideos #tanzaniatrendingstory #TanzaniaTre #madeintanzania🇹🇿 #madeintanzan #madeintanzania #SupportLocal #madeintanzaniat #roadto100followersontwitch #madeintanzaniawith #chawamata_tv #viraltz
CHAWAMATA TV
Region: TZ
Thursday 17 September 2026 07:28:11 GMT
Music
Download
Comments
akayoha og :
naona Kuna mpango wa kubadili gia angani
2026-09-17 08:13:27
57
J4 :
Makosa ya gari mpeni mwenye gari yakwangu kiuendeshaji nipeni mimi
2026-09-17 08:18:21
31
zuberi_mchilima13 :
point za nn kwani kuna ligi ya madeleva
2026-09-17 08:11:46
48
E E 16689 :
ponti hata Kenya zipo ila sio makosa ya kuovatek au kutowasha ta, ponti inakatwa pale inapo tokea ajali kubwa ya kuua kwauzembe,
2026-09-17 08:28:22
27
king muubay 24 :
chamsingi madereva hakuna kuingia rodi bhana
2026-09-17 11:11:18
3
lusekelonelson1 :
oyooooooo line hiii
2026-09-17 09:46:04
0
USTADHI WA TANZANIA :
hizi point zimaisha tu, ina maana dereva yeye hashindi tuwe tunapata point
2026-09-17 10:32:47
4
mmojawapo :
[Laugh approved][Laugh approved][Laugh approved] political
2026-09-17 07:42:42
0
rj magar :
mbn me nimekatw
2026-09-17 08:54:57
0
Kimoda :
kwani hii nchi ikoje mbona wanatuona mashwain
2026-09-17 08:19:34
8
Tamimu Update :
toeni tu
2026-09-17 09:13:19
0
Jose Paroko :
29 tena
2026-09-17 10:19:32
0
Richie :
fungeni vifaa maalumu vya kurekodi makosa barabarani hii itasaidia sana
2026-09-17 08:32:14
7
Hemedi Baruti ngoma :
atutaki
2026-09-17 08:50:09
0
peterkulwa982 :
neno POINT hatutaki kulisikia kwenye Resen zetu
2026-09-17 10:43:41
2
fadymoses 🚚 Truck driver ✔️ :
mpango waku felisha September 29
2026-09-17 09:31:34
3
Nelson Majaliwa :
me jana imeandikwa fain mbili zinaonyesha remain 13 point
2026-09-17 09:04:49
0
👑 KiBELLa oG :
HAPA JESHI LA POLICE WANAKINZANA WENYEWE KWA WENYEWE SASA 🤔🤔🤔
RSA KULE WANAENDELEA NA KUTUKANDAMIZA KWA KUTUMIA CLIP ZA TRAFFIC WA KIGOMA KATIKA KITUO KIMOJA
2026-09-17 08:10:41
5
lastborn :
kama hazina madhara sasa ni za NN??
2026-09-17 09:02:45
1
💥 𝗪𝗔𝗦𝗘𝗟𝗔 𝗦𝗠𝗔𝗥𝗧𝗬👣 :
Me jana kosa moja wamenikata points 6 zikabaki 9 kisa stika ya nenda kwa usalama na gari ni ya kampuni nilipiga hadi goti kuwaomba lakini haikusaidia
2026-09-17 13:51:29
1
Seif Rashid :
Alafu tuna bunge hii sheria ime tokea wapi ata hatujui
2026-09-17 08:37:11
0
jamse mwangi :
Mbona tulikuwa tunapewa faini hakuna points
2026-09-17 08:30:40
4
Charles Michael :
we mbona unauwa nyota haitolewe
2026-09-17 08:33:18
2
Ghost General trainer 🔥 🇹🇿 :
naona hapo ni mm tu sijaelewa kwenye maelezo hayo
2026-09-17 08:40:22
0
SAMDU :
acheni kutuonea madereva .mnataka tufanye kazi gani.kwa nini madereva nchi hii
2026-09-17 09:29:34
4
To see more videos from user @chawamata_tv, please go to the Tikwm
homepage.