@centikcydxw: #vivonu #lymphdrainagekapseln #gesund #fpy #tiktokshop

Ztwfl wzdxtl
Ztwfl wzdxtl
Open In TikTok:
Region: DE
Thursday 17 September 2026 07:53:39 GMT
746
2
0
2

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @centikcydxw, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos

Ilikuwa ni Alhamisi. Saa nne asubuhi. Nilikuwa nimeanza kazi zangu za kawaida hospitalini. Ghafla simu ya ofisi ikaita. Nikaipokea. Iikulikuwa ni sauti ya mwanaume. Sauti yake ilikuwa nzito. Lakini ndani yake kulikuwa na wasiwasi ambao hata yeye mwenyewe alikuwa anajaribu kuuficha. “Doctor…” “Ndiyo.” “Nakuomba usiondoke hospitalini.” “Kuna mtoto wangu nataka nimlete.” Nikamuuliza: “Kuna tatizo gani?” Akanyamaza kwa sekunde kadhaa. Kisha akasema: “Hatujui.” “Kwa miezi mingi amekuwa akiumwa.” “Anachoka sana.” “Hana nguvu.” “Anapungua uzito.” “Na jana usiku hali ilibadilika zaidi.” Nikamuambia mlete. Baada ya kama dakika arobaini hivi… gari kubwa likaingia hospitalini. Mzee akashuka. Pembeni yake kulikuwa na kijana mmoja wa makamo ya miaka 22. Mwanafunzi wa chuo. Mwembamba. Uso wake ulikuwa umechoka sana. Alionekana kama mtu ambaye alikuwa hajalala vizuri kwa muda mrefu. Pembeni yao alikuwepo kijana mwingine mdogo. Mwanafunzi wa kidato cha tano. Niliwaingiza ndani. Nikaanza kuchukua historia. Mwanzoni baba yake ndiye aliyekuwa anaongea. Alinieleza jinsi mtoto wake alivyokuwa akirudi kutoka chuo akiwa mchovu. Jinsi alivyokuwa anapata homa za mara kwa mara. Jinsi alivyokuwa akilala muda mwingi. Jinsi walivyokuwa wakidhani ni stress za masomo. Lakini kadri muda ulivyopita… hali ilizidi kuwa mbaya. Baada ya muda nikamuomba kijana mwenyewe aongee. Akanitazama. Kisha akasema: “Doctor…” “Mimi nachoka sana.” “Hata nikitembea umbali mfupi nahisi nimekimbia kilomita nyingi.” “Napata homa mara kwa mara.” “Nimepungua uzito.” “Sina nguvu kama zamani.” Alikuwa anaongea huku macho yake yakiwa yamechoka. Nikaendelea na uchunguzi. Nikashauri tufanye vipimo mbalimbali. Baba yake akakubali. Vipimo vikafanyika. Muda ukapita. Matokeo yalipoanza kuonekana… moyo wangu ukawa mzito. Kulikuwa na jambo ambalo sikulitegemea. Nilimuita kijana pembeni. Nikaanza kuzungumza naye kwa utulivu. Kadri mazungumzo yalivyoendelea… macho yake yakaanza kuwa mekundu. Kisha ghafla akaanza kulia. Kilio kikubwa. Kilio cha mtu ambaye anajutia kitu. Nilimpa muda. Baadaye nikamuuliza: “Je, kuna jambo lolote ungependa kuniambia?” Akafuta machozi. Kisha akasema: “Doctor…” “Usimwambie baba yangu kwanza.” Nikamwambia: “Sawa.” Kisha akaanza kusimulia. Polepole. Kwa sauti iliyokuwa inatetemeka. Aliniambia kuwa miezi kadhaa iliyopita… Alikuja binti mmoja nyumbani kwao. Binti mdogo. Mwenye heshima. Mwenye sura ya upole. Alikuwa ametoka kijijini. Alikuwa amepata kazi ya ndani kupitia ndugu zake. Mwanzoni alikuwa mfanyakazi tu. Lakini kadri muda ulivyopita… akawa rafiki yake mkubwa. Walikaa pamoja. Waliongea. Walicheka. Kwa sababu kijana huyo alikuwa mpweke sana. Hakupenda marafiki wengi. Hakupenda kutoka ovyo. Mtu aliyekuwa karibu naye zaidi alikuwa yule binti. Mpaka siku moja… wakajikuta wamevuka mipaka. Wakafanya mapenzi. Na baada ya hapo… wakawa karibu zaidi. Alipomaliza kusimulia… akaangalia chini. Kisha akasema:  “Doctor… Mimi nishakufa Daah ..! ” Baada ya mazungumzo yale… nikamuita baba yake. Nikazungumza naye kwa utulivu. Mzee alikaa kimya muda mrefu. Muda mrefu sana. Kiasi kwamba nilihisi hata kupumua kulikuwa kumemshinda. Lakini mwisho akasema: “Naomba nimlete huyo binti.” Siku iliyofuata… walimleta. Alikuwa mdogo sana. Mwembamba. Mpole. Na alikuwa analia tangu aingie hospitalini. Nilipozungumza naye… alikubali kuwa alikuwa karibu sana na yule kijana. Vipimo vikafanyika. Na yeye pia akagundulika kuwa ameathirika. Lakini hapo ndipo sehemu iliyoniumiza zaidi . Kwa sababu baada ya mazungumzo marefu… binti akaanza kusimulia historia yake. Akasema: “Doctor…”  “Kabla sijaja mjini nilikuwa na mchumba.” Akaanza kulia. “Tulikuwa tumepanga kuoana.” “Lakini nilipopata kazi huku…”  “mawasiliano yakapotea.”  “Mwisho tukaachana.” Akaendelea kulia. “Mimi sikujua chochote.”  “Sikujua hali yangu.”  “Sikujua nilikuwa nimebeba maumivu ambayo yangekuja kuwagusa watu wengine.” Nilinyamaza. Kwa sababu wakati mwingine hakuna wa kulaumiwa. Kuna watu tu wanaokutana katikati ya majeraha ambayo hawakuyachagua. Lakini bado hadithi haikuwa imeisha. Baada ya siku mbili… #swahilitiktok  #tiktoktanzania🇹🇿🇹🇿🇹🇿  #tiktokkenya🇰🇪🇰🇪🇰🇪

About