@mkuraysh: Aliyekuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar Kawambwa pamoja na masheikh wengine wawili wamekutwa na makosa kufuatia uchunguzi uliofanywa na Tume Maalumu iliyoundwa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania na Mwenyekiti wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ali. Akiwasilisha ripoti ya Tume hiyo leo, Katibu wa Tume, Dkt. Abdallah Tego, amesema uchunguzi ulihusu makosa ya kimaadili na kiuongozi, ambapo Tume ilikusanya nyaraka mbalimbali, zikiwemo taarifa za mitandaoni, kufanya mahojiano ya ana kwa ana na kwa njia ya simu na mashahidi, wakiwemo viongozi waliofanya kazi kwa karibu na masheikh hao, pamoja na kupokea maelezo yao ya utetezi. Hata hivyo, Tume imesema Sheikh Walid Alhad Omar Kawambwa, hakuitikia wito wa kufika mbele ya Tume kwa ajili ya kutoa utetezi wake, licha ya juhudi zilizofanywa na Tume kumtafuta. Kwa upande wa Sheikh wa Mkoa wa Singida, Sheikh Issa Nassor Issa, na Sheikh wa Mkoa wa Kigoma, Sheikh Hassan Idi Kiburwa, Tume imesema waliitikia wito na kufika mbele yake kwa ajili ya kutoa utetezi. Kwa mujibu wa Tume, maelezo yao yalisaidia kupunguza uzito wa baadhi ya makosa yaliyokuwa yakiwakabili. Tume imewasihi Masheikh hao kusikiliza na kuheshimu uamuzi utakaotolewa na Baraza la Ulamaa, ikieleza kuwa hatua hizo zinalenga kulinda maslahi ya umma wa Kiislamu. Aidha, imeutaka umma kuwa mtulivu wakati ukisubiri uamuzi wa mwisho wa Baraza la Ulamaa.

mkurayshsaudiya
mkurayshsaudiya
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 17 September 2026 08:57:42 GMT
36302
533
42
5

Music

Download

Comments

mwadiniothman
mwadiniothman :
kilakitu kina mwisho tutafika mwisho wetu tutakutana na mwenye ulimwengu wake Allah tusamehe mazambi yetu mpeuvumilivu na subra shekh waalid
2026-09-17 11:36:18
11
abdul.yusuph37
Abdul Yusuph :
shekhe Walidi Kalinga heshima yake maana anae takiwa kunyenyekewa na mwenyezi mungu peke yake na hao mashekhe eti kisa kutaka cheo cha ushekhe mkuu wa mkoa kama alikuwa na kila mtu kaona weledi wake hayo mengine kwao ni chuki na fitna ila mungu anajuwa ukweli kuhusu shekhe Walid
2026-09-17 16:28:59
6
user4797341368826
bosslady :
alaf hakuna mkamilifuu tukianza kuchunguzaaa kla mtu ana lake kosa awe abubakar zuber wala awe nan kla mtu amewahi fany kosa msichukulie kam fimbo ya kuwaadhibu wengne allah pekee ndo anafaham ukwel wa mamb yote hli linakwaza n kuwadhalilisha viongoz wa dini namtak alyevperfect ambaye hajawah kukosea ata robo aje dm nna mzigo wake hebu acheni hzoo mshawah sikia upande wa pili wanafany hv kwann sisiii tuacheee jmn inakwazaa😭😭😭
2026-09-17 16:10:40
2
jumahamisi431
jush ragna :
Allah akupe subra mm najua Sheikh Walid ni walli min auliyai Allah
2026-09-17 15:30:30
2
user9161681171098
user9161681171098 :
maana halis ya mwanaadam n mtu mwenye kukosea so at sh walid pia nimwanadam hajakamilik kwaiy kukosea kwake pia kumeumbw hata mitume yetu pia ilimkosea mola wetu
2026-09-18 02:38:19
0
amour.bey
Amourly..☆ TZ :
astaghafirullah...yaani mashekh ndio mmefkia huku
2026-09-17 10:54:17
2
ummu_zey
Royals Queen. :
Allah atawashinda
2026-09-17 15:18:59
1
khadijajuma598
@Khadija :
mimi kila siku nazidi kuumia 😭😭😭
2026-09-17 20:42:58
0
haloomy_de_lawyer1
Ayam♥️ :
Utetezi wa nn na hukumu mulishaitoa ???
2026-09-17 19:41:53
0
puzzled672
Puzzled :
wasije tu kumfungia sheikh wetu kufanya kazi ya Mungu
2026-09-17 17:51:12
0
kadabra423
kadabra :
2026-09-17 19:13:31
0
toneysterwarty
Tz landscaper :
KUNA HAJA GANI
2026-09-17 22:06:52
0
user32533814704861
user32533814704861 :
mdogo wangu walidi uko vizuri 🙏🙏🙏 siku nyingine wakikuteua kataa bado una mambo mengi yakufanya
2026-09-17 19:55:04
0
ramadhani.swelele
ramadhani swelele :
mungu ampe sheke walid maisha marefu leompaka yaumull qiyama🙏🙏
2026-09-17 18:40:39
0
ally_nyota_graphics
Ally_Nyota Decorations ✨ :
Yeye shekh walid anajua Allah ndio mjuzi wa kila jambo na yeye kasha muachia yeye hana haja ya kujitetea Kwa wanadamu ambao hawana chakumpa Wala pakumpeleka kesho yaumul kiyama
2026-09-17 21:03:13
0
zuu1790
Ummy Haitham :
Sasa alishatuhumiwa na hiyo kesi bado wanamtaka nn sheikh anachokwenda kutoa ushahid ni kitu gani au akishafika ofisini ndo atarudishwa kwenye cheo chake wamuache aendelee na harakati zake mungu ndo kila kitu atamsimamia
2026-09-17 18:07:23
0
user4797341368826
bosslady :
duuhh wallahy mtihan yaaan siku hzi dini imegeuzwa kuwa siasa subhnallah😭😭..mashaallah shekh walid nmepnd ulichofany
2026-09-17 16:08:03
1
mwadiniothman
mwadiniothman :
Katika nyie hapo nani masafi mungu atupe hatma njema amin
2026-09-17 11:25:12
0
mwadiniothman
mwadiniothman :
shekh mziwanda alisema mnatutisha waislam kwa vyeo hiyo ni zamana tu
2026-09-17 11:27:45
0
dullahmtaita
dullah Mtaita :
mollah tupe uvumilivu
2026-09-17 13:34:27
0
yusuph.said61
Yusuph Said :
sisi tunaamini Kila jambo hua lime andikwa na Allah kwaiyo kama waiailam nasheha walidi nimuisila alitu shtui ilo naukizingatia uongozi nidhima
2026-09-17 15:59:07
0
mwadiniothman
mwadiniothman :
mungu analipa kwa nia si matendo
2026-09-17 11:32:09
0
fauzia.bamatraf3
fauzia bamatraf :
mashaallah shekh walid allah maak
2026-09-17 21:13:51
0
hassan.j.h
Hassan j h :
kumtegemea Allah kwa kila jambo, mungu ni muweza na ni mjuzi wa kila jambo ni imamani yangu yuko pamoja nao na haki itatendeka
2026-09-17 15:33:38
0
user2828113785495
user2828113785495 :
Yaani hakuna sababu za msingi lakin ALLAH ndiye hakimu wa haki basi
2026-09-17 16:15:30
0
To see more videos from user @mkuraysh, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About